Madiwani
wa halmashauri mbili ya Mji na Wilaya ya Geita pamoja na watumishi mbali mbali
wakifuatilia kikao taarifa na maadhimio juu ya kikao ambacho kinaendelea.
Mkuu wa
Wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi ambaye ndiye Mwenyekiti wa kamati za ulinzi
na usalama akielezea juu ya hatua hizo ambazo zimechukuliwa na mabaraza hayo.
Mbunge wa
Geita ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Joseph Kasheku
Msukuma,akielezea na kuunga hoja ambayo imetolewa na wajumbe.
Mwanasheria wa
Halmashauri ya Mji wa Geita ,Akisoma taarifa na maadhimio juu ya Mgodi wa GGM.
Baraza maalum la madiwani lililojumuisha Madiwani wa Halmashauri ya Mji
na Wilaya ya Geita limesema hawako tayari kushirikiana na mgodi wa dhahabu wa
Geita, GGM hadi mgodi utakapokuwa tayari kuwalipa Dola milioni 12,645,345.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwepo kwa madai yatokanayo na kodi ya huduma
kutoka mgodi wa dhahabu wa GGM, madai ya kuanzia mwaka 2004 hadi 2013.
Hali hiyo imesababisha madiwani wa Halmashauri zote mbili kukutana kwenye
kikao ambacho kimewahusisha watendaji wa halmashauri zote, wananchi na afisa
kutoka mgodi wa GGM na kuutaka mgodi huo kusitisha huduma za jamii
ambazo walikuwa wakizifanya pamoja na magari ya kampuni hiyo
kutotumia barabara za Halmashauri hizo pamoja na kuzuia huduma ya maji kufika
kwenye mgodi huo.
Magulu Kuzenza ambaye ni diwani wa kata ya Bukondo, Elias Ukumu Diwani wa
Nyachiluluma na Bi Amina Swedi Kanijo wameeleza kuwa hawawezi kuendelea
kuubembeleza mgodi huo
Akisoma taarifa ya kamati ya Mkuu wa Mkoa ya wafanyabiashara Kaimu
Mwenyekiti wa TCCIA John Luhemeja ameelezea mapendekezo ya kamati hiyo juu ya
namna ambavyo wamewaza kubaini ujuma ambazo zinafanywa na mgodi huo.
“Tumefatilia tukabahini kuwa kuna ujuma ambazo zimeendelea kufanywa na
baadhi ya watendaji wa mgodi wa GGM kwa kushindwa kutoa fursa za ajira kwa
maeneo haya na mwisho wa siku kujikuta wanatoa ajira kwa watu wa
kanda ya kasikazini ikiwemo swala la tenda hivyo tunaamini tamko letu la leo
litatoa mstakabari juu ya mambo ambayo yanafanywa na mgodi”Alisema Luhemeja
Kutokana na mapendekezo ambayo yametolewa ya mgodi kutokupitisha magari
yake kwenye Halmashauri hizo Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na
usalama Wilayani Humo ambaye ni Mkuu wa Wilaya hiyo,Mwl Herman Kapufi amesema
kuwa hatawaandikia barua GGM wasipitishe magari kwaajili ya usalama na pia
hatatoa taarifa kwa mkuu wa mkoa juu ya mgogoro uliopo kwenye halmashauri hizo.
Kwa upanda wake Meneja mwandamizi wa mahusiano kwenye mgodi huo Manase
Ndoloma ,amesema kwa upande wao wanaheshimu mabaraza yote mawili na kwamba kwa
swala la hilo surusheni yake ni mahakamni na kwamba wapo tayari
kwenda mahakamni kwani ndio chombo pekee ambacho kinatoa haki .
Utekelezwaji wa agizo hilo unatarajia kuanza kesho muda wa saa sita za
usiku kwa kuzuhia magari kuingia kwenye halmashauri zote mbili na bomba ambalo
lipo Rungwe kufungwa.
No comments:
Post a Comment