Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe katika Kitabu cha Usajili pamoja na
Simu kuashiria Uzinduzi wa Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto
waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara leo 26 Septemba,
2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiwakabidhi vyeti Wazazi
kwa niaba ya watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa Uzinduzi wa
Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano
leo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara 26 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbalimbali wanaosaidia
Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano
mara baada ya kuuzindua leo Wialayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, 26 Septemba,
2017.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kwa niaba ya Waziri
wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. John Palamagamba amezindua Mpango wa Usajili na
Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Mtwara na
Lindi.
Uzinduzi huo
umefanyika leo katika Viwanja vya Matogolo Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara
ukiwa na lengo la kuwasajili watoto waliochini ya umri miaka mitano pamoja na
kuwapatia vyeti ambavyo vitawasaidia kutambulika kwao na kisha kupewa nyaraka
za uthibitisho yaani vyeti vya kuzaliwa.
Waziri Mwakyembe
amesema kwamba, katika kupanga maendeleo ya nchi kunahitajika takwimu sahihi za
matukio muhimu za Watanzania ambazo zinaelezea taarifa zao za kuzaliwa ikiwemo
za vifo kwakuwa takwimu hizo zinasaidia kujua mahitaji ya wananchi katika sekta
mbalimbali ikiwemo afya, elimu, lishe pamoja na sehemu nyinginezo.
“Mpango huu utaondoa
utegemezi wa takwimu za kuhisia, takwimu za kukadilia ndugu zangu mfumo
tulionao sasa unategemea Sensa ambayo hufanyika kila baada ya miaka 10, na
matukio bado yanatokea, hivyo kutumia Mpango huu kutasaidia kupata takwimu
sahihi na halisi za Watanzania wote”, alisema, Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa, Mikoa
ya Lindi na Mtwara itanufaika na mpango huo kwakuwa Serikali itakuwa inatambua mahitaji
halisi ya wananchi kupitia taarifa zitakazochukuliwa za uandikishaji wa watoto
hao, huku akisisitiza kuwa, anaamini kwamba mikoa hiyo itakuwa chachu ya
kuongezeka kwa idadi ya watoto watakaoandikishwa kama ilivyofanyika katika
baadhi ya mikoa mingine ya Tanzania.
Kwa upande wake Katibu
Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Prof. Sifuni Mchome amesema kwamba kama
Wizara wana wajibu wa kufikisha huduma hiyo kwa wananchi hususani kwa wananchi
ambao wako maeneo ya mbalibila kujali hali yao ya kimaisha huku akisisitiza
kwamba kila mtoto atapatiwa haki hiyo ya kuandikishwa na kupewa cheti hivyo.
“Kila mtoto mwenye
umri chini ya miaka mitano ana haki ya Kikatiba ya kupewa huduma hii, hivyo
tutahakikisha kwamba kila mtoto katika Taifa letu anapewa huduma hii bure
kupitia RITA”, alisema Prof. Mchome.
Naye Kaimu Afisa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), Bibi Emmy
Huddson amesema kwamba, mpango huo umeanza kutekelezwa leo katika
mikoa hiyo miwili ikiwa ni mwanzo wa utatuzi wa changamoto ya upatikanaji wa
haki ya mtoto ya kutambuliwa kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto ya Mwaka 2009 pamoja
na Mikataba mbalimbali ya Kimataifa na Kikanda ambayo Tanzania kama nchi
imeiridhia.
Amebainisha kuwa,
mpango huo haumaanishi kwamba hapo awali huduma hiyo ilikuwa haitolewa
isipokuwa huduma hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo
kutofika kwa huduma hiyo kwa wakati jambo lililosababisha watoto wengi
kutosajaliwa kwa watoto na kupatiwa vyeti vyao vya kuzaliwa kwa wakati.
“Kupitia huduma hii,
watoto wataweza kupata uthibitisho wa tukio la kizazi au cheti cha kuzaliwa
ambacho ni nyaraka muhimu inayomwezesha mtoto kupata huduma mbalimbali kama
nchini kama vile ajira, afya, elimu pamoja na huduma na nyinginezo, niwaase
wakazi wa Mtwara na Lindi kutumia vyeti hivyo badala ya kutumia Viapo au
maelezo ya mdomo”, alisema Bibi Emmy.
Mpango wa Usajili na
Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano nchini unatekelezwa na
Ofisi ya Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) ambao
unasimamiwa na Wizara ya Katiba na Sheria, ambapo hapo awali ulianza
kutekelezwa katika mkoa wa Dar es Salaam na baadaye ikafuata mikoa ya Mbeya,
Mwanza, Iringa, Njombe, Geita, Shinyanga ambapo hivi leo mikoa ya Mtwara na
Lindi inajumlisha idadi ya mikoa kufikia tisa.
No comments:
Post a Comment