Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya
Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga
(kushoto) akiongea wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip
Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini
Dodoma, Kulia ni Mjumbe wa Bodi hiyo
Prof. Sufian Bukurura.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga
wakati wa makabidhiano ya Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha
2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya
Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga
akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya
Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
akikata utembe baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa
Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
akionesha kwa wanahabari na wajumbe wengine wa Bodi(hawapo pichani) kitabu cha
Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, ,
Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Manunuzi ya Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
akiongea na wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya
Umma (PPRA) baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa
Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma ambapo ameahidi kuzichukulia hatua taasisi
zote zilizokiuka taratibu za manunuzi zilizoainishwa kwenye Ripoti ya Tathmini
ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.
Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa
Manunuzi ya Umma (PPRA) Dkt. Laurent Shirima akiongea,
wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya
Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya Udhibiti wa
Manunuzi ya Umma (PPRA).
Hayo yamesemwa leo Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango
alipokuwa akipokea ripoti ya tathimini ya utendaji wa Taasisi za Serikali katika sekta ya
Manunuzi iliyofanywa na PPRA kwa mwaka wa Fedha 2016/17.
“Tutazichukulia hatua na kuziwajibisha taasisi zote
ambazo zimebainika katika ripoti hii kuwa na viashiria vya rushwa au kufanya malipo yenye utata katika manunuzi yao,”
alisema Dkt. Mpango.
Dkt. Mpango amesema kuwa, zaidi ya 70% ya fedha za
Umma zinatumika kununua vifaa na huduma mbalimbali hivyo Serikali haitavumilia
kuona fedha hizo zinatumika bila kufuata sheria na kanuni zilizowekwa.
Aidha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa PPRA
Balozi Dkt. Matern Lumbanga amezitaja taasisi ambazo zimekiuka sheria na
taratibu za manunuzi kwa mwaka 2016/2017 kuwa ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),
Taasisi ya Mifupa (MOI) pamoja na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taasisi nyingine ni Shirika la Bima la Taifa (NIC),
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),
Mamlaka ya Anga (TCAA), Wizara ya Fedha na Mipango na Halmashauri ya Wilaya Kondoa.
Balozi Lumbanga amesema kuwa uchunguzi wa zabuni mbili
zenye thamani ya shilingi bilioni 160.5 ambazo zilikuwa zinatekelezwa na Wizara
ya Fedha na Mipango pamoja TCAA haukubainika mapungufu ya msingi na PPRA
ilipendekeza utekelezaji wa miradi hiyo uendelee kama ilivyopangwa.
“Uchunguzi uliofanywa katika taasisi sita zilizobaki
ulibaini kuwa Serikali ilipata hasara ya takribani shilingi milioni 12.15
kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo, ucheleweshaji wa malipo kwa wakandarasi
uliosababisha ongezeko la riba pamoja na faini zilizotokana na ukiukwaji wa taratibu
za kijamii na mazingira kabla ya kuanza kwa utekelezaji wa kazi za ujenzi,”
alisema Balozi Lumbanga.
Balozi Lumbanga amezitaja Taasisi zilizobainika na
malipo yenye utata kuwa ni Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL) na Halmashauri ya Kwimba. Ukaguzi wa kupima upatikanaji
wa thamani ya fedha ulibaini malipo yenye utata katika taasisi hizo tatu ambazo
ni kiasi cha shilingi milioni 483.44 zililipwa kwa wakandarasi kwa kazi ambazo
hazikuwa zimefanyika.
Vile vile amesema kuwa, miradi 33 katika taasisi 17
ilibainika kuwa na kiwango kikubwa cha viashiria vya rushwa. Taasisi hizo ni
Mamlaka za Maji Safi na Maji Taka za Moshi (Muwasa), Mwanza (Mwauwasa) na
Arusha (Auwasa) pamoja na Halmashauri ya Wilaya za Wilaya za Msalala, Kibondo
na Moshi.
Taasisi byingine ni Taasisi ya Sayansi na Teknolojia
ya Nelson Mandela, Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Chuo cha Ufundi Arusha,
Halmashauri ya Mjia wa Kahama, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya
Uhasibu Arusha (IAA), Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Kilimanjaro, Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Halmashauri ya Mji wa
MAsasi pamoja na Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).
Ripoti hiyo ni ripoti ya 11 kuwasilishwa Wizara ya
Fedha na Mipango tangu PPRA ilipoanzishwa.
No comments:
Post a Comment