Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia
baadhi ya picha za Mashujaa wa Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati
alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za
Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe (kushoto) akionyeshwa ramani iliyotumika wakati wa Ukombozi nchini
Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la Naliendele kwenye mnara wa
Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison
Mwakyembe (kulia) akiangalia bango linaloelezea kumbukumbu za Mashujaa wa
Ukombozi waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara
eneo la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba,
2017.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe
(kushoto) akiangalia mchanga wa makaburi yaliyofukuliwa ya Mashujaa wa Ukombozi
waliopigana Vita nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo la
Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akiangalia
moja ya silaha za kivita iliyotumiwa na Mashujaa wa Tanzania wakati wa
Vita vya Ukombozi nchini Msumbiji wakati alipotembelea Mkoani Mtwara eneo
la Naliendele kwenye mnara wa Kumbukumbu za Mashujaa hao 25 Septemba, 2017.
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amelipongeza Jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kuhifadhi vema kumbukumbu za Mashujaa wa Tanzania
waliopigana vita na kusaidia ukombozi katika baadhi ya nchi za jirani ikiwemo nchi
ya Msumbiji.
Pongezi hizo amezitoa
leo Mkoani Mtwara wakati alipotembelea maeneo ya kumbukumbu ya Kitaifa ambapo
kwa Mkoani hapo ametembelea eneo la Mashujaa lililopo Nailendele lengo likiwa
ni kujionea maeneo yaliyoweza kuhifadhiwa kumbukumbu zake za ukumbozi wa Bara
la Afrika ikiwemo mahitaji ya ziada ya maeneo hayo.
Mhe. Mwakyembe amesema
kwamba, kazi kubwa inayofanyika katika kuyatembelea maeneo hayo ni kujua
kumbukumbu za maeneo hayo ikiwemo kuongea na mashuhuda wa matukio ya kumbukumu
za maeneo husika kwa ajili ya kuandika historia ya Afrika kwa ushahidi
uliotafutwa na Waafrika wenyewe.
“Tunakipinid kifupi
kuhakikisha kuwa kumbukumbu zote tuizonazo tunazihifadhi, tunaandika historia
yetu sisi wenyewe Waafrika badala ya kuandikiwa na Waliotutawala huko nyuma kwa
ushahidi tulioutafuta wenyewe”, alisema Dkt. Mwakyembe.
Ameongeza kuwa JWTZ
imefanya kazi kubwa ya kuhifadhi baadhi ya maeneo ya kumbukumbu za kitaifa,
jambo ambalo litarahisisha utunzaji wa kumbukumbu hizo kwa ajili ya Mradi wa
Ukumbozi wa Bara la Afrika.
“Tumeanza kukubaliana
wote katika SADC na katika nchi za Afrika, ni lazima tuingize katika mitaala ya
shule zetu hizi harakati za ukombozi wa Bara la Afrika ili vizazi vijavyo
viweze kufahamu mambo haya hususani tulikotoka na tunakoelekea”, alisema Dkt.
Mwakyembe.
Aidha, katika ziara
hiyo Mhe. Mwakyembe alipata wasaa wa kuongea na Uongozi wa Mkoa wa Mtwara
ambapo ameupongeza kwa uongozi huo kwa kuja na Mpango wa Usajili wa Vizazi vya
Watoto waliopo chini ya Umri wa Miaka Mitano ambapo Uzinduzi huo unatarajiwa
kufanyika kesho Wilayani Tandahimba.
No comments:
Post a Comment