Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga Akizungumza na walimu wakati wa Kongamano ambalo limeandaliwa na NMB Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita.
Baadhi ya walimu ambao wanatoka kwenye halmashauri zilizopo Mkoani Geita wakifuatilia Hotuba ya Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga.
Meneja wa Benki ya NMB Mkoani Geita Mathias Nkuliwa akizungumza wenye Kongamano hilo ambapo alisema lengo la kungamano hilo ni kutambua mchango wa walimu katika Benki ya NMB.
Meneja wa NMB Kanda ya ziwa Abraham Augustino akizungumza na walimu wakati wa
Kongamano.
Meza Kuu ikiongozwa na Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita wakimsikiliza meneja wa kanda wakati alipokuwa akizungumza.
Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga Akizungumza na walimu wakati wa Kongamano ambalo limeandaliwa na NMB Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita.
Baadhi ya wafanyakazi wa NMB wakisikiliza maelezo ya Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga wakati akizungumza kwenye Kongamano hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ambaye alikuwa Mgeni Rasmi akifungua Kongamano la walimu na Benki ya NMB ambalo limefanyika kwa mala ya kwanza Mkoani Geita.
Baadhi ya wadau wa idara ya Elimu Mkoani Geita wakimtegea sikio Mgeni Rasmi. wakati alipokuwa akizungumza na walimu pamoja na wafanyakazi wa NMB Mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa NMB.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa Elimu wa Wilaya mbali mbali zilizopo Mkoani Geita.
Mkuu wa Mkoa wa Geita akiondoka na kuagana na Wafanyakazi wa NMB baada ya kuwa amefungua Kongamano hilo.
Imebainika kuwa bado kuna idadi kubwa ya watanzania wasiotumia mifumo rasmi ya kifedha na kibenki , ambapo tafiti zinaonesha zaidi ya asilimia ishirini (20) ndio wanaotumia huduma za kibenk huku sababu kubwa ya kutokutumia ni ukosefu wa elimu na ufahamu wa kutosha kuhusu huduma za Kibenk.
Akizungumza na Walimu ambao walikuwa kwenye kongamano la siku
ya walimu Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga amesema
kuwa ipo sababu ya kuvishawishi vyombo vya kifedha na taasisi nyingine husika
kuwa na program maalumu za kutoa Elimu ya masuala ya kifedha hususani maeneo ya
vijijini.
“Hivyo basi kuna kila sababu ya kuvishauri vyombo vya fedha na taasisi
nyingine husika kuwa na program maalumu za kutoa elimu ya masuala ya kifedha
hususani maeneo ya vijijini ili watanzania walio wengi zaidi waweze kunufaika
na maendeleo yaliyofikiwa na sekta ya fedha hapa nchini”Alisema Kyunga.
Aidha kwa upande wake Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na
Mauzo wa NMB Omar Mtiga amesema kuwa idadi ya watanzania karibia milioni
50 ni asilimia 20 tu ndio wenye akaunti za benki , na zaidi ya
asilimia 60 ya wananchi wanamiliki simu za mkononi na wana uwezo wa kufanya
malipo na miamala kupitia simu za mkononi.
“NMB kwa sasa inaamini katika kutoa huduma za kibenki za kidigitali kwa
watanzania wote ,njia hii tunaiona ni bora zaidi na inaendana na kasi ya ukuaji
wa teknolojia na itasaidia kuleta mwamko mkubwa zaidi kwa watanzania wengi
kuweza kutumia huduma za kibenki kwa kufanya miamala na malipo mbali
mbali”Alisema Mtinga .
Mtinga ameendelea kuelezea kuwa wateja walionao ni zaidi ya
milioni 2.5 kati yao zaidi ya wateja milioni 2 wanatumia simu za mkononi
kufanya miamala na kuangalia salio ,kufanya malipo mbalimbali kama kulipia
umeme hata kulipia kodi mbalimbali.
Aidha kwa upande wake Mwalimu Imani Amisi ameelezea kuwepo kwa changamoto
kubwa ya kimikopo hususani katika taasisi za Kifedha kuwepo kwa riba
kubwa hali ambayo inasababisha wengi wao kushindwa kukopa fedha hizo lakini
kutokana na maelekezo ambayo wamepatiwa na NMB wanaamini kuwa Benki hiyo
itakuwa mkombozi katika maswala ya Mikopo.
No comments:
Post a Comment