Mbunge wa Jimbo la Geita ambaye ni mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi Mkoani Geita ,Joseph Kasheku Msukuma akizungumza na
wananchi jimboni kwake
Kamanda wa Jeshi la Polisi
Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo Akizungumza na waandishi wa Habari juu ya
tukio la kuandamana wa madiwani wa Halmashauri mbili za Mji na Wilaya.
Amesema kuwa Mbunge huyo wamemkamata majira ya mchana mjini Geita na
kwamba wanaendelea na mahojiano ambayo yatasaidia kuwabaini wale ambao
walihusika na tukio.
Kamanda Mponjoli amesema jeshi lake linaendelea na msako wa
kuwabaini,kuwakamata na kuwachukulia hatua wale wahusika wa tukio hilo na
kwamba sheria ya makosa ya jinai hayana kikomo na kwamba mtu
akifanya kosa leo na akakwepa ataendelea kutafutwa,na hana namna ya kuukwepa
Mkono wa sheria.
Mapema wiki hii ,jeshi hilo lililazimika
kutumia nguvu kutawanya maandamano ya madiwani pamoja na wananchi walioweka
vizuizi katika barabara inayoingia mgodini wakishinikiza kulipwa ushuru wa
huduma kiasi cha dola za kimarekani milioni 12.65 sawa na zaidi ya shilingi
trillion 26.
No comments:
Post a Comment