Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Sheikh
Abdurahman Muhamed Ame (kushoto) akielezea juu ya Mkutano wa 48 wa Jumuiya hiyo
mbele ya waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 September hadi 1 Oktoba leo jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya hiyo Tahir Mahmood Chandhry.
Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Tahir Mahmood Chandhry (katikati) akifafanua
jambo juu ya Mkuatano Mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo mbele ya waandishi wa habari
unaotarajiwa kufanyika tarehe 30
September hadi 1 Oktoba, leo jijini Dar
es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi
wa Jumuiya ya hiyo Sheikh Abdurahman Muhamed Ame, Kulia ni Katibu wa
Uchapishaji wa Jumuiya hiyo, Jamil Mwanga.
Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Tahir
Mahmood Chandhry (katikati) akisoma barua iliyotumwa na Khalifatul Masihi Mkuu
wa Jumuiya hiyo duniani Mirza Mansoor Ahmad mbele ya waandishi wa habari
kuelekea katika Mkutano Mkuu wa 48 utakaofanyika tarehe 30 September hadi 1 Oktoba mwaka huu,
leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam
ya Ahmadiyya Tanzania Sheikh Abdurahman Muhamed Ame. Kulia ni Kulia ni Katibu wa Uchapishaji wa Jumuiya
hiyo Jamil Mwanga.
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Msaidizi
wa Jumuiya hiyo Sheikh Abdurahman Ame alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo
alisema kauli mbiu ya mkutano huo ni, “Muislam wa kweli ni yule ambaye watu
wengine wote wako salama dhidi ya shari ya ulimi wake na mikono yake.”
Kauli mbiu hiyo inawaasa waislam duniani kote kwamba, wana haja ya kuishi na kutenda kwa namna
ambayo watu wengine watakuwa mashahidi kwamba Islam ni dini ya amani.
“Mkutano huo siyo wa kisiasa wala si mkutano dhidi
ya madhehebu mengine duniani bali unawakumbusha waumini wa kiislamu juu ya masuala
na wajibu wao wa kidini,” alifafanua Sheikh Ame.
Aidha, alisema kuwa jumuiya hiyo ndiyo pekee
miongoni mwa jumuiya za kiislam iliyo na utaratibu wa ukhalifa ikiongozwa na kiongozi
mmoja anayesimamia utendaji katika kila nchi duniani kote. Hapa nchini jumuiya
hii ina upekee kwani ndiyo ya mwanzo kutafsiri Qurani tukufu kwa lugha ya
Kiswahili mwaka 1953.
“Jumuiya hii imekuwa ikifanya mikutano yake mikuu
kila mwaka kwa lengo la kukumbusha misingi sahihi ya dini tukufu ya Islam,
kukuza udugu na urafiki miongoni mwa wana jumuiya na wananchi kwa ujumla na
kuhamasisha uwepo wa amani katika jamii,” alieleza Sheikh Ame.
Akiwakilisha barua ya kiongozi mkuu wa jumuiya hiyo
duniania aitwaye,Hadhrat Mirza Mansoor Ahmad, Amir na Mbashiri Mkuu wa jumuiya
hiyo hapa nchini Tahir Chandhry, aliwasilisha alieleza kuwa washiriki hawana
budi kuliombea taifa amani na kujizatiti katika kuienzi jumuiya kwa maendeleo ya dini ya uislam duniani kote.
“Ninawahimiza nyote mjizatiti kutimiza masharti ya
baiat zenu hususan kuienzi taasisi ya
kiroho ya Khilafat-e-Ahmadiyy. Jueni ya kwamba maendeleo ya Jamaat, kuenea kwa
Islam na kupatikana kwa amani duniani, kimsingi vinaambatana na taasisi ya
Ukhalifa,” alieza Chandhry.
Aidha aliongeza kuwa, ni wajibu kwa kila mwananchama
wa jumuiya hiyo popote alipo duniani anapaswa
kuonesha mapenzi, nguvu na wajibu wao
katika kuchangia maendeleo ya taifa hili na kufanya kila kinachowezekana
kudhibiti madaraka yao.
“Hivi ni kama vita kila mmoja anapaswa kuwa mzalendo
katika nchi yake, kutii katiba na
kufanya mambo ya maendeleo kwa ajili ya taifa letu, kwani bila amani hakuna
haki,” alieleza Chandhry.
Jumuiya ya Ahmadiyya ilianzishwa na Hadhrat Mirza
Ghulam Ahmad a.s wa Qadian India mwaka 1889, nchini Tanzania ilisajiliwa rasmi
mwaka 1934 ambapo mbali na kutoa huduma za kiroho imekuwa mstari wa mbele kutoa
huduma za kijamii pasipo kujali itikadi za wananchi.
Huduma ambazo zimekuwa zikitolewa na jumuiya hii
ni kuchimba visima vya maji, huduma za
afya pamoja na elimu ya sekondari katika Mkoa wa Dar es Salaa na elimu ya awali
na msingi katika mkoa wa Morogoro pia jumuiya hiyo ipo katika hatua za mwisho
za uanzishaji na ukamilishaji wa kituo cha radio nchini.
Jumuiya
Ahmadiyya ni ya kimataifa iliyoenea
katika nchi 210. Mkutano wa mwaka huu utahudhuriwa na washiriki kutoka nchi za nje za Kenya,
Uganda, Burundi, Malawi, Msumbiji na Uingereza.
No comments:
Post a Comment