Baadhi ya askari wa kikosi cha kutuliza Ghasia wakiwa kwenye Barabara
ambayo inatoka mgodi wa dhahabu wa Geita GGM Wakati wa shughuli za kuwatawanya
viongozi hao pamoja na wananchi ambao walikuwa wameandamana .
Wananchi na madiwani wakiwa wameweka Mawe kabla ya kutawanywa
.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita,Elisha Lupuga
akiwa kwenye kikao wakati alipokuwa akielezea namna ambavyo wameweza kufukuzwa
na jeshi hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl, Herman Kapufi akizungumza na
kutoa maelekezo ya namna ya kufanya wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya
wakati alipokuwa akiwakilisha maamuzi ambayo wameyachukua.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga
akiwasisitiza kutulia na kuachana na ghasia wasubilie meza ya mazungumzo na
Naibu waziri wa Nishati na madini siku ya Jumatatu.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Geita Mponjoli Mwabulambo
akisisitiza kutokukubaliana na madiwani juu ya tukio ambalo wamefanya siku ya
leo.
Jeshi la Polisi Mkoani Geita limelazimika kutumia mabomu ya machozi na
kupiga risasi za moto hewani kwaajili ya kuwaondoa waandamanaji ambao walikuwa
wakiongozwa na madiwani wa halmashauri mbili ambazo ni ya mji na Wilaya ya
Geita ambao walikuwa wametanda kwenye barabara ya mgodi huo wakizuia magari
kuingia na kutoka Kampuni ya uchimbaji madini ya dhahabu ya Geita
(GGM),wakishinikiza kulipwa deni wanaloidai GGM kiasi cha zaidi ya Dola Bilioni
12.65
Tukio hilo limetokea leo (jana) majira ya saa mbili na nusu asubuhi
wakati madiwani hao na wananchi wakiwa wamefunga barabara ya mgodi
wakishinikiza kulipwa deni hilo kufuatia maazimio ya kikao maalumu cha baraza
la madiwani kilichokeiti juzi.
Azma ya kukata mawasiliano ya barabara na vyanzo vya maji zilianza saa
10.00 usiku ambapo madiwani waliweka mawe katika njia kuu za kuingia mgodini
humo na kwenye chanzo cha maji kilichopo Nungwe.
Baadi ya madiwani ambao wamzungumza na Maduka online Joseph kwenye eneo
la tukio baada ya kutawanywa na mabomu ya machozi Sasembe
Kaparatusi na Constantine Molandi ambaye ni makamu mwenyekiti wa
halmashuri ya mji wa Geita wamesema kuwa walikubaliana jana (juzi)
kwenye vikao vya chama ngazi ya wilaya na mkoa pamoja na baraza
maalum kuwa leo watafanya maandamano ya amani kwa lengo la kushinikiza
kudai deni hilo huku wakilaani kitendo cha jeshi hilo kutumia nguvu kubwa.
“Tulikubaliana kwenye vikao
ngazi ya chama wilaya ,na mkoa na baraza maalum la madiwani na
uongozi wa wilaya pamoja na mkoa unafahamu kuwa leo
tunaandamana kudai haki lakini cha kushngaza askari polisi
wametutawanya kwa mabomu “ alisema Kaparatus .
Kabla ya kutawanywa waaandamanaji hao,Mbunge wa jimbo la Geita Bw. Joseph
Kasheku Msukuma ameiambia maduka online kuwa amesikitishwa na Kamanda
Mkuu wa Polisi kumtuhumu kuwa yeye ndiye mchochezi mkuu wa mgogoro huo.
“Nashangaa sana RPC anakuwa na chuki na mimi kwani kuwa Mbunge ni tatizo
kwani ubunge alinipa yeye hata kama nikiacha ubunge nina maisha yangu na awezi
kusema kuwa ccm ni kielele yani kweli sisi ni kielele”alisema Msukuma.
Ameonezea kuwa kiasi cha fedha zinazodaiwa zinatakiwa kulipwa
kwani zimekuwa za muda mrefu na zinaweza kusaidia katika swala la maendeleo.
Hata hivyo amemtaka Kamanda Mponjoli kuomba radhi kwa Chama Cha
Mapinduzi ccm na kwa serikali kwa ujumla kutokana na kauli mbaya
alizotoa, akiongeza kuwa ameidhalilisha chama hicho.
“Kwa kauli hiyo inadhihirisha wazi kuwa Polisi wanakuwa na upande wakati
wanapoenda eneno la kazi na hilo halitakiwi na kwa kutuuliza kwa dhihaka iwapo
sisi ni CCM ama siyi, hiyo kauli ni mbaya sana kwani sisi tulikuwa tukidai haki
ya kodi hiyo kwa niaba ya wananchi wetu.
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga, ambaye
aliwalaumu madiwani hao kwa kitendo cha kukata bomba la maji katika chanzo cha
maji cha Nungwe, aliingilia kati suala hilo akashauri kuwa ni vyema shauri hilo
likamalizwa kwa kutumia busara kwa manufaa ya wana Geita.
“Waheshimiwa Madiwani tuweke mbele hekima na busara, tuweke mbele huduma
za jamii, za mgodi wa GGM na wananchi kwa jumla ziendelee kwa amani hebu
tuwe watulivu wakakti tukitafuta suluhu, kudai haki ni sawa lakini ni njia zipi
mnatumia kuzidai, tuache kudai haki kwa njia ya fujo ya aina hii kwani sheria
za nchi haziruhusu,”alisema.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Geita Mwl..Herman Kapufi amesema suala
hilo limefikishwa katika wizara ya nishati na madini na kwamba jumatatu ya wiki
ijayo Naibu waziri akiambatana na Kamishina wa madini watafika mkoani Geita
kukutana na pande zote kwaajili ya kutafuta suluhu
“Hata hivyo tumewasiliana na Naibu
Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Mendrad Kalemani juu ya suala hili
ambapo tumekubaliana kukutana jumatatu ijayo, akiambatana na Kamishna wa madini
ambapo tutakaa nao pamoja na GGM ili kujadili suala hili”Alisema Kapufi.
Licha ya ahadi hiyo ya Viongozi kutoka kwenye wizara husika, Mwenyekiti
wa chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Geita Barnabas Mapande akaomba kutoa
taarifa kwa mkuu wa wilaya kuwa kamanda wa jeshi la Polis mkoani humo
anawatetea wawekezaji hasa GGM ambao wameshindwa kulipa fedha za kuharakisha
maendeleo ya Mkoa
Naye Mkuu wa mkoa huo Meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga,amesema njia
pake
e ya kumaliza mgogoro huo ni kufuata sheria,kanuni na taratibu bila
kuathiri shughuli za kijamii na huduma kwa wananchi na kwamba njia iliyotumiwa
na madiwani kudai haki yao si sahihi.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa
Geita,Mponjoli Mwabulambo amesema hayupo tayari kuomba radhi kwani swala hilo
na mkusanyiko huo umefanyika kinyume cha sheria na kwamba hakuna lugha ambayo
ametumia kukikashifu chama cha mapinduzi CCM.
No comments:
Post a Comment