Serikali imewasilisha
Mkataba wa Kimataifa wa Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika
Mashariki kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya
Jamhuri ya Muungano.
Akiwasilisha Mkataba
huo kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amesema
kuwa Tanzania na Uganda ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambayo
malengo yake ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya nchi wanachama kwenye
maeneo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii kiteknolojia , utafiti, ulinzi na masuala
ya Kisheria.
Dkt. mwakyembe amesema
kuwa Serikali ya Uganda kupitia kampuni za Kimataifa za TOTAL, TULLOW NA CNOOC
iligundua uwepo wa mafuta ghafi takribani mapipa bilioni 6.5 katika eneo la
Albertine nchini Uganda.
" Kufuatia
ugunduzi huo, Serikali ya Uganda ilianza kutafuta njia ya kusafirisha mafuta
hayo kwenda kwenye soko la kimataifa ambapo iliaanisha njia takribani tatu
ikiwemo ile ya kutoka Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini
Tanzania" amesema Dkt. mwakyembe.
Aidha Dkt. mwakyembe
amebainisha baadhi ya faida zitokanazo na Mkataba huo ikiwemo kuongezeka kwa
mapato ya Serikali kutokana na Kodi ya zuio na Kodi ya Mapato ya Kampuni
zitakazotozwa wakati wa ujenzi na uendeshaji wa Mradi.
Vilevile amesema kuwa
Serikali ya Tanzania itanufaika katika kuongezeka kwa mapato ya Serikali kwa
takribani Dola za Marekani 12.2 kwa kila pipa la mafuta ghafi
litakalosafirishwa kupitia Bandari ya Tanga kulingana na kiwango cha Hisa za
Serikali ya Tanzania.
" kuimarika kwa
mahusiano ya kidiplomasia, ulinzi na usalama kati ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Jamhuri ya Uganda pamoja na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa
ujumla sambamba na kuimarika kwa huduma mbalimbali katika bandari ya Tanga
kutokana na shughuli za Mradi na miundombinu itakayojengwa" aliongeza Dkt.
Mwakyembe
Pia ongezo kwa fursa
za ajira kwa Watanzania ambapo takribani watanzania 10, 000 wataajiriwa
wakati wa ujenzi na ajira zipatazo 1,000 wakati wa uendeshaji, Amesema Dkt.
Mwakyembe.
Kwa upande wake
Deogratius Ngalawa akimuwakilisha Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge
ya Nishati na Madini ameishauri Serikali kuhakikisha inasimamia utekelezaji wa
mkataba huo kwa kuzingatia mustakabali wa manufaa ya kiuchumi kwa Taifa.
" Napenda kutoa
pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa juhudi zake na umahiri aliouonesha katika kuhakikisha Tanzania
inapata fursa ya mradi huu mkubwa wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta
ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga, Tanzania" Amesema Ngalawa.
Akiongea
kwa niaba ya Msemaji Mkuu kambi Rasmi ya Upinzani Wizara ya Nishati na Madini
Mhe. Devota Minja amesema kuwa bomba hilo la kusafirisha mafuta ilikuwa na kazi
iliyohusu zaidi ushawishi mpana kwani kulikuwa na ushindani mkubwa utoka kwa
nchi jirani.
No comments:
Post a Comment