Monday 20 February 2017

ZAIDI YA NYAVU HARAMU 495 ZIMEKAMATWA WILAYANI CHATO



Zaidi ya nyavu haramu  495 zenye thamani  ya milioni  85  laki mbili na elfu 78 zimekamatwa wilayani chato  mkoani geita katika msako mkali ulioongozwa  na maafisa uvuvi  pamoja na mkuu wa  wilayani hiyo kwa lengo la kutokomeza uvuvi haramu ulioshamili katika ziwa victoria
Wilaya ya chato ni sehemu ambayo ina idadi kubwa  ya wavuvi wa samaki ambapo  kuna jumla ya wavuvi 3336  na mitumbwi  1112  pamoja na  mialo 36  kutokana na hilo kumekuwepo na baadhi ya wavuvi ambao hawafuatai sheria na taratibu za uvuvi na badala yake kukiuka na kuanza kutumia uvuvi haramu kitendo ambacho kinaweza kupelekea  kutokomeza samaki katika ziwa victoria.

Kutokana na hilo viongozi pamoja na baadhi ya wavuvi  wameweka mpango mkakati wa kuhakikisha suala hilo wanalishughulikia kikamilifu ili kutokomeza uvuvi haramu  ulio kithiri katika eneo hilo.
Wakizungumza baadhi ya viongozi wa wavuvi  wamepongeza juhudi za viongozi wa eneo hilo kwa kukamata  nyavu haramu katika eneo hilo kwani bila kufanya hivyo    wimbi la wavuvi haramu linge kuwa linaongezeka  kila kukicha.

Kwa upande wao  maafisa uvuvi Bi.Damali Charles pamoja na Makisensio Masasi katika kata ya Nyamirembe wilayani chato wamesema watapambana kikamilifu ili kuhakikisha wanatokomeza suala la uvuvi haramu wilayani humo.


Aidha mkuu wa wilaya ya chato  Bw. Shabani Ntarambe amesema  kutokana na agizo hilo kupewa na makamu wa raisi  wa Jamhuri ya muungano wa  Tanzania  Bi. Samia Hassan la kuhakikisha anamaliza uvuvi haramu katika eneo hilo, suala hilo atalivalia njuga na kwa kiongozi yeyote katika wilaya hiyo atakae shinndwa kutimiza majukumu yake kwa wakati kuhusiana na zoezi hilo la kupambana na uvuvi haramu hatua kali za sheria zitachukuliwa dhidi yake.

No comments:

Post a Comment