Saturday 4 February 2017

WATUMISHI WANNE HALMASHAURI YA NYANG'HWALE WATUMBULIWA



Watumishi wanne wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita wamesimamishwa kazi kwa tuhuma  mbalimbali

Kikao cha Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya nyang’hwale kilichofanyika  Februari mosi na 02  kimewasimamisha kazi watumishi wanne wa idara mbalimbali wilayani humo, mara baada ya kupatikana na tuhuma  katika utendaji wao.

Akiwataja watumishi hao mwenyekiti  wa halmashauri hiyo Aloyce Mussa Lumambi,amesema baadhi ya watumishi hao,ni pamoja na wakuu wa idara mbili Bw. Donatus Pangani  ambaye alikuwa mkuu wa idara ya fedha na Dayness Mosha aliyekuwa mkuu wa Idara elimu  ya Sekondari.

Mkuu wa wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gwiyama amelipongeza Baraza hilo na ameongezea kuwa  bado kuna baadhi ya watumishi wanafanya kazi bila kufata maadili ya kazi zao huku akitoa onyo kwa wale ambao hawatojali maslahi ya wananchi.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Carlos Gwamagobe amekiri kusimamishwa kwa wafanyakazi   hao. 

No comments:

Post a Comment