Thursday 2 February 2017

WTUMISHI WA MAHAKAMA MKOANI GEITA KUTOA HAKI KWA MISINGI NA SHERIA



Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa  mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Sheria mkoani Geita 

Jamii ya wanasheria Mkoani Geita  imetakiwa kutoa haki kwa misingi na sheria ikiwa ni pamoja na kuzingatia swala la muda kwenye kesi ambazo wanazisimamia.
Kauli hiyo imesemwa na wakili wa serikali Mkoani humo Emily Kiria  wakati wa maadhimisho ya wiki ya sheria, ambapo ameeleza kuwa jamii ya wanasheria  wote wawe wa serikali na wakujitegemea wanajukumu la kuhakikisha wanatoa haki kwa uharisia na ukweli kwa swala usika.

Jamii ya wanasheria na hili ni jukumu la wanasheria wote wawe wa serikali au wa kujitegemea wanalo jukumu la kuhakikisha wanatoa haki kwa uharisia na kwa ukweli wa swala usika na siyo kuhakikisha tu kwamba wanawatetea au kuwasaidia watu kwasababu tu wamefika kuomba msaada”alisema Kiria

Kwa upande wake wakili kutoka chama cha mawakili Tanzania(Tanganyika law society),Bernad Otieno,alifafanua kuwa  mahakama inawajibu wa kusikiliza malalamiko yanayoletwa na wananchi na kuyatolea mahamuzi wajibu huo ni wa kikatiba kwani inatokana na jamhuri ya mwaka 1977 kama ilivyofanyiwa marekebisho katiba ibara ya 107 (A) ibara ndogo ya kwanza na ya pili.

Mkuu wa Mkoa wa Geita ambaye alikuwa  mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo ,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,ameendelea kusisitiza swala la muda wa kusikiliza kesi ,pamoja na  kuwataka watumishi wa mahakama  kuwa wahadilifu na waaminifu kwenye shughuli zao.

Naomba kutoa wito kwa watumishi kuendesha kesi kwa muda usika ikiwa ni pamoja na kuwa waaminifu katika shughuli zenu za kila siku za kutoa haki kwa wananchi”alisisitiza Kyunga


Siku ya Sheria nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na Mahakimu ili kuweza kusikiliza kesi  ambapo kitaifa imefanyikia jijini Dar es salaam na Mgeni Rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli,kauli mbiu ikiwa ni Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.

No comments:

Post a Comment