Wednesday 1 February 2017

RC GEITA AAGIZA WAKUU WA WILAYA KUTUNZA MAZAO NA CHAKULA KILICHOPO MKOANI GEITA



Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,akitazama nafaka kwenye soko la ccm Kata ya katoro.




 Mkuu wa Mkoa wa Geita,Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,akitoa agizo la kuakikisha chakula kinalindwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bukombe.

Mkuu wa Mkoani  wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ,amewaagiza  wakuu wa wilaya wote kuhakikisha wanasimamia vyakula  vilivyopo ikiwan ni pamoja na kudhibiti uhuzwaji wa  nafaka kwenye wilaya  na mikoa jirani.
Mh. Kyunga ametoa maagizo hayo wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea maghala ya vyakula kwenye wilaya za Geita,Bukombe na Mbongwe lengo likiwa ni kujionea hali ya chakula Mkoani humo

Amesema kuwa ni vyema kwa wakuu wa wilaya kudhibiti chakula  kilichopo ikiwa ni pamoja na kuwaelekeza wananchi kutunza mazao katika kipindi hiki ambacho mvua zimekuwa ni za kusuasua

Niwaombe wakuu wa wilaya zote kuwa waangalifu na kukilinda chakula kilichopo ili Wilaya na Mikoa ya jirani isije ikachukua na kutuacha hatuna tena chakula lazima hiki kilichopo kitunze na kuhifadhiwa na muwahimize wananchi walime mazaa ambayo yanakubaliana na mvua kidogo Mfano,Viazi Mtama na muhogo”Alisema Kyunga 

Akisoma taarifa ya mazao na hali ilivyo kwasasa kwenye soko la kibiashara Katibu wa wafanya Biashara Soko la CCM Kata ya Katoro, Charles Mlale alisema  kuwa Bei ya nafaka kwa mwaka huu imepanda zaidi ikilinganishwa na mwaka jana kwani mwaka jana Gunia la mahindi walikuwa wanachukulia kiasi cha Sh. elfu themanini kwa sasa imefika kiasi cha laki na ishirini


Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya  Mkuu wa wilaya ya Bukombe Josephat Maganga  amemhakikishia Mkuu wa Mkoa kufanyia kazi maagizo aliyoyatoa ikiwa ni pamoja na kuakikisha hakuna mtu ambaye hatatoka mikoa ya jirani au wilaya kuja kununua mazao yaliyopo kwenye wilaya wanazozisimamia .

No comments:

Post a Comment