Monday 13 February 2017

WAKAZI WA CHATO MKOANI GEITA KUBORESHA VYOO VYAO VYA ASILI



Baadhi ya wakazi wilayani Chato mkoani geita wametakiwa kuboresha vyoo vya asili  kuwa vya kisasa kutokana na  mvua za masika kuanza kunyesha ili kuepuka  vyoo hivyo kutitia na kusababisha magojwa  ya milipuko  yanayo weza kujitokeza kutokana na uchafu wa vyoo hivyo .
Rai hiyo imetolewa  na Mwenyekiti wa kijiji cha Mapinduzi  Bw.Kitute  Kalegea kijijini hapo  ambapo amesema kuwa  kuna idadi kubwa ya wakazi katika  eneo hilo ambao wanatumia vyoo vya asili ambavyo  haviwezi kudumu  kwa muda mrefu kutokana na miundo mbinu yake kujengwa kwa kutumia udongo pamoja na miti.

Kalegea amewataka wananchi  ambao hawana  vyoo katika  kjijini hicho wachimbe mara moja kwani  kume kuwepo na baadhi  ya wakazi katika eneo hilo ambao hawana vyoo katika familia zao na badala yake huduma hiyo huipata katika vichaka vilivyo jiranai na nyumba zao jambo ambalo ni hatari kwa afya zao pamoja na kijiji kizima kwa ujumla.


Aidha baadhi ya wakazi  katika kijiji hicho wamesema kuwa  kumekuwepo na idadi kubwa ya watu ambao wanatumia vyoo vya asili jambo ambalo  ni hatari kutokana na vyoo hivyo kutitia wakati wa mvua za masika zinapo anza kunyesha kitendo ambacho kinawafanya watumiaji wa huduma hiyo kukosa sehemu rasmi ya kujisaidia na badala yake  wengine  kutumia mifuko  ya plasitiki  kwa kujikimu na mifuko hiyo mara nyingi hutupwa    kando kando ya vyanzo vya maji pamoja na barabara kitu  ambacho kinaweza kusababisha magonjwa  ya milipuko kwa baadhi ya wakazi katika kijiji hicho. 

No comments:

Post a Comment