Tuesday 28 February 2017

18 WAKAMATWA KWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA GEITA


  

Kamanda wa polisi mkoani Geita mponjoli mwabulambo akiongea na  waandishi wa habari.
Jumla ya watuhumiwa 18 wamekamatwa  na Jeshi la polisi mkoani Geita kwa kujihusisha na  biashara ya madawa ya kulevya aina ya bangi, watuhumiwa hao  wamekamatwa kwa nyakati tofauti  katika msako mkali unaondelea mkoani hapa.

Katika msako huo eshi la polisi limekuta baadhi ya watu wakiwa wamelima bangi maeneo ya makaburi, ambapo wameteketeza mashamba hayo huku wengine wakikutwa na magunia pamoja na misokoto  ya madawa hayo ya   kulevya.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema kuwa watu hao wamekamatwa katika kipindi cha mwezi february mwaka huu.

Aidha amesema zoezi hilo ni mwendelezo ndani ya mkoa huo wakite-keleza agizo la serikali kuhakikisha wanatokomeza madawa   ya  kulevya.


Baadhi ya waliokamatwa akiwemo Athanas John wametaja maeneo ambayo wamekuwa wakihusika kuuzia wakati alipokuwa akihojiwa na mkuu wa upelelezi wa Jeshi la polisi Mkoa wa Geita Allan Bukumbi.

No comments:

Post a Comment