Saturday 4 February 2017

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI YAISHAURI SERIKALI KUINUA SEKTA YA KILIMO



Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndasa 

Sekta ya Kilimo inachangia ajira takribani asilimia 70 ya Watanzania ambapo imekuwa ikitegemewa kusaidia kufanikisha juhudi za kupunguza umaskini hasa Vijijini na kuchochea mapinduzi ya Viwanda. Kwa mwaka 2015 ukuaji wa sekta hiyo ulikuwa ni 

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Josephat Kandege ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akisoma taarifa ya utekelezaji ya kamati hiyo kwa kipindi cha mwezi Januari 2016 hadi Januari 2017.

Kandege amesema kuwa sekta hiyo imekuwa ikitegemewa na watanzania wengi katika kuwaingizia kipato na hata kuinua uchumi wa Nchi, lakini wakulima wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali katika Sekta hiyo kama vile gharama kubwa ya pembejeo, ukosefu wa masoko ya uhakika na idadi ndogo ya wataalamu wa Kilimo.

“Kamati inaishauri Serikali kuanza kutekeleza mikakati madhubuti ya kuinua sekta hii kwa kuboresha kilimo cha umwagiliaji, kuboresha  teknolojia ya Kilimo, kuwezesha uanzishwaji wa viwanda vingi vya usindikaji wa mazao ya kilimo na kusambaza maafisa ugani wa kutosha katika maeneo yote ya nchi,” alisema Kandege.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndasa amesema kuwa Kilimo kinahitaji uwekezaji mkubwa hivyo ni vyema Serikali ikawekeza katika sekta hiyo kikamilifu ili kuinua uchumi wa Nchi na mtu mmoja mmoja. 

Akijibu hoja hizo, Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Ole Nasha amesema kuwa Wizara hiyo imejipanga kupambana na changamato za pembejeo ambazo zimekuwa zikipatikana kwa gharama ya juu maeneo mengi nchini.

Hata hivyo amesema kuwa wizara hiyo iko katika mkakati wa kuanza kuzalisha mbolea ndani ya nchi ili kupunguza gharama ya mbolea na ili iweze kuuzwa kwa bei moja nchi nzima.

No comments:

Post a Comment