Friday 10 February 2017

WANANCHI WA KATORO WAIOMBA SERIKALI KUWEKA VIGINGI KATIKA TAASISI ZA SERIKALI



Baadhi ya wakazi wa mtaa wa afya katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na mkoani Geita wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Aridhi nyumba na maendeleo ya makazi kuweka vigingi katika Taasisi za Serikali zilizopo karibu na makazi ya watu  mtaani hapo ili kuepuka  hasara inayo weza kujitokeza hapo baadae  ya kubomolewa nyumba zao.
Wakizungumza na storm habari baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema kuwa  wanaiomba  Wizara ya  Ardhi , nyumba  na maendeleo ya makazi kufanya  vipimo vya ardhi  katika  taasisi za serikali pamoja na makaazi ya watu ili kuepuka  hasara za kubomolewa nyumba zao hapo baadae

Kwa upande  wake  mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Masaga Misso ameiomba  Wizara husika kufika katika eneo hilo kwani kuna maeneo makubwa ya watu  ambayo yamezunguka taassisi za Serikali na hayajafanyiwa  vipimo .


Masaga misso amesema kama Serikali itaweka mpango mkakati wa kupima viwanja vya wananchi pamoja na serikali katika  mtaa huo itaondoa migogoro ya ardhi ambayo inaweza kujitokeza hapo baadae.

No comments:

Post a Comment