Saturday 4 February 2017

CCM WILAYANI GEITA CHAADHIMISHA MIAKA 40










Chama  cha mapinduzi (CCM) Wilayani  Geita kimeadhimisha miaka arobaini  (40)  tangu kuanzishwa  kwake  mnamo februari,  mwaka 1977 kwa kufanya shughuli ya ujenzi wa kituo cha Afya kwenye Kata ya shiloleli  iliyopo  Halmashauri  ya mji wa Geita.

Akizungumza  na  wananchi kwenye  shughuli hiyo ya ujenzi  wa kituo cha Afya mwenyekiti wa CCM Wilayani hapa , Barnabas Mapande amemwambia  Muhandisi kusimamia kwa umakini ujenzi wa  Boma  isije kutokea tatizo baada ya kuwa umemalizika Ujenzi.

Diwani wa kata ya Shiloleli,  Bonface  Kaswahili ameelezea pamoja  na ujenzi  huo kuendelea bado wanakabiliwa na changamoto ya upungufu wa maji ya kujengea jengo hilo.

Kwa upande wa baadhi ya wananchi ambao wamezungumza  na  Storm habari  kuwa kukamilika ujenzi wa Kituo hicho  cha  Afya kutarahisisha safari  ya  muda  mrefu kutembea kufuata  huduma na kina mama wajawazito kujifungulia   njiani.


Aidha Katibu Mwenezi wa Chama hicho, Jonathani Masele ameeleza kuwa Chama hicho kitaendelea  kujitolea  kwa shughuli  za wananchi ili kufata  Ilani  ya uchaguzi ya mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment