Wednesday 1 February 2017

TSH. MILIONI 15 ZATOLEWA KWA VIJANA WALIOFUKIWA NA KIFUSI GEITA


Jumla ya kiasi cha Tsh. milion 15   zilizotolewa na watu mbalimbali wilaya na mkoa wa geita,kwa ajili ya kuwapa pole vijana 15 walifuokiwa na kifusi  january 26 kwenye mgodi wa RZ zimekabidhiwa na mkuu wa wilaya ya Geita mapema  leo.
Akikabidhi  fedha  hizo mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi  amesema kuwa  watu  ambao wamechangia  fedha hizo ni  9 wakiwemo Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani pamoja  na mbunge wa Jimbo la Busanda Bi. Laurencia  Bukwimba.

Msemaji  wa  Mgodi  huo  na Mwanasheria  Francis Kiganga,ameendelea kuwashukuru  wadau wote ambao wamejitolea kwa hali na mali  huku meneja  wa Mgodi  Giu  Liu  pia  ametoa shukrani kwa watanzania wote ambao wamejitolea kwa hali na mali kutoa msaada wakati wa matatizo kwenye   mgodi  huo.


Anisent  Masanja akiwawakilisha waathirika wenzake ameahidi kufanyia kazi  fedha  ambazo wamepatiwa katika suala la maendeleo na amewaomba watu ambao wameshiriki kuwatoa kwenye machimbo hayo kuendelea na moyo wa kujitolea  kwani  kufanya hivyo mungu  atawabariki.

No comments:

Post a Comment