Tuesday 7 February 2017

AUWAWA KWA KUPIGWA NA WANANCHI MKOANI GEITA KWA KUSADIKIKA NI MWIZI



Mtu mmoja asiye tambulika kwa jina wala makazi na anaye kadiliwa kuwa na umri wa  kuanzia miaka 24 na kuendelea amekutwa amefariki kandokando ya barabara iendayo shule ya sekondari Lutozo katika mamlaka ya mji mdogo wa Katoro Wilayani na Mkoani geita .
Akizungumza Mwenyekiti wa mtaa wa Afya Bw. Masaga Misso  ambapo mwili  huo umeonekana amesema kuwa tukio hilo limetokea  jana majira ya saa kumi  na moja Alfajiri  ambapo mtu huyo alishambuliwa  na Wananchi wenye hasira kali  kwa kusadikika kuwa ni mwizi wa mahindi pamoja na mihogo mashambani.

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la Jadi (sungusungu) wa  mtaa huo Bw. Mashaka Venas  amewataka Wananchi katika eneo hilo kuto jijengea tabia ya kuchukua sheria mkononi pindi wamkamatapo mtu kwa tuhuma yeyote.


Aidha baadhi ya wakazi walio shuhudia mwili huo wamewataka vijana kuachana na tabia ya wizi na badala yake wajishughulishe katika shughuli ndogongogo zinazo weza kuwa patia kipato ambacho kina weza kuwaondoa katika mawazo mabaya kama ya wizi, utumiaji wa  madawa ya kulevya na mambo mengine yafananayo na hayo.

No comments:

Post a Comment