Wednesday 15 February 2017

WAUZAJI WA SAMAKI WILAYANI CHATO WAIOMBA SERIKALI KUPUNGUZA GHARAMA YA KUPATA LESENI



Wafanya biashara wa samaki wilayani Chato mkoani Geita wameiomba serikali kupunguza bei ya kuchukulia lesseni ya  kuendesha  shughuli hiyo ya uzaji wa samaki kutokana na bei hiyo kuwa  juu zaidi .
wakizungumza jana baadhi ya wafanya biashara katika soko la chato mjini  wamesema kuwa   kumekuwa na changamoto nyingi katika uendeshaji wa biashara hiyo wilayani  humo kutokana na ushuru ulio kithiri jambo ambalo limepelekea baadhi ya wafanya biashara kukimbia soko hilo.

wafanya biashara hao wameiomba serikali kupitia halmashauli ya wilaya ya chato kupunguza kodi  zisizo kuwa za lazima ili kuweza kufanya biashara hiyo kwa kufuata misingi na taratibu zitakazo wafanya kunufaika na biashara hiyo.


kwaupande wake mwenyekiti wa soko hilo bw. Daudi Francisco ameiomba Serikali kuliangalia na kulifanyia kazi suala hilo  kwani  hali hiyo inasababisha kupunguza mapato katika eneo hilo kutona na baadhi ya wafana biashara kuacha kufanya biashara hiyo  kwa sababu ya kodi zilizo kithiri .

No comments:

Post a Comment