Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wakiongea na mmoja ya wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha
wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika
Manispaa ya Tabora mkoani Tabora Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Aggrey Mwanri na
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe. Queen Mlozi wakati yeye na Mama Mary
Majaliwa walipotembelea katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao na
ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary
Majaliwa wakiongea kwa furaha na wazee wasiojiweza wanaolelewa katika kituo cha
wazee na watu walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika
Manispaa ya Tabora mkoani Tabora Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mama
Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa pamoja na meza kuu
wakipata picha ya kumbukumbu na vijana na watoto wenye ulemavu wa ngozi
waliokaribishwa kwenye hafla katika kituo cha wazee na watu walemavu watokanao
na ugonjwa wa ukoma cha Amani Ipuli katika Manispaa ya Tabora mkoani Tabora leo
Februari 15, 2017
Mke wa Rais Mheshimiwa
Mama Janeth Magufuli na Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa wametoa wito kwa
Watanzania kujengea utamaduni wa kutembelea vituo vya wazee na watu wenye
mahitaji maalumu na kutoa misaada ili waweze kujikimu.
Wameyasema hayo leo
(Jumatano, Februari 15, 2017) wakati walipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza
na walemavu watokanao na ugonjwa wa ukoma ya Amani Ipuli yaliyoko kwenye
Manispaa ya Tabora mkoni Tabora.
Katika makazi hayo
wamekabidhi tani 7.5 za vyakula mbalimbali ukiwemo mchele, unga wa sembe na
maharage pamoja na mafuta maalumu kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa ngozi
wanaosoma katika shule mbalimbali mkoni Tabora.
Hata hivyo, Mama
Janeth amewapongeza watumishi wote wanaofanyakazi kwenye makazi ya kulelea
wazee na watu wenye mahitaji maalumu kwa sababu kazi hiyo ni ngumu na ina
changamoto nyingi.
“Ibada si kwenda
katika nyumba za ibada pekee bali hata kuwatembelea wazee, watu wenye mahitaji
maalumu na wasiojiweza utakuwa umetoa sadaka kubwa kwa Mwenyezi
Mungu. Nawaomba tujitahidi kuwatembelea,” alisema.
Kwa upande wake Mama
Mary amewaomba wananchi wote wawe na utaratibu wa kuwasaidia wazee wanaoishi
katika makaazi ya kulele wazee, walemavu na wasiojiweza nchini na kuwafariji
kwa sababu wanahitaji upendo na faraja kutoka kwao.
Pia Mama Mary
ameipongeza Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja
na wadau mbalimbali kwa kujitoa kwa hali mali katika kuwahudumia wazee na watu
wenye mahitaji maalumu.
Naye Naibu Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangala amesema
Serikali itahakikisha huduma zinaboreshwa katika makazi ya kulelea wazee na
watu wenye mahitaji maalumu nchini kwa kuwa vingi viko katika hali mbaya.
Awali Ofisa Ustawi wa
Jamii mkoa wa Tabora, Bw. Baraka Makona alisema makazi hayo yalianzishwa mwaka
1969 kwa lengo la kuwasaidia watu wasiojiweza hususan walioathirika na ugonjwa
wa ukoma ambao walitengwa na familia zao.
Bw. Makona alisema
baada ya ugonjwa wa ukoma kupungua mkoani Tabora kwa sasa makao hayo
yanahudumia wazee wasiojiweza wenye ulemavu na ambao wametengwa na jamii
kutokana na sababu mbalimbali.
Katika hatua nyingine, Bw. Makona alisema makazi hayo yanakabiliwa na changamoto
mbalimbali zikiwemo za uchakavu wa majengo, ukosefu wa gari la wagonjwa hali
inayosababisha usumbufu mkubwa hasa inapotokea dharura nyakazi za usiku kwani
hakuna zahanati karibu na makazi hayo.
Pia Bw. Makona
amewapongeza wake wa viongozi hao kwa moyo wao wa dhati wa kuamua kutembelea
makazi hayo na kutoa misaada mbalimbali vikiwemo vyakula kwa sababu wameonyesha
matendo ya huruma na Mwenyezi Mungu atawabariki.
Naye Mwenyekiti wa
Wazee waishio katika makaazi hayo, Mzee George
Busambilo aliwashikuru wake hao wa viongozi kwa niaba ya wenzake na
kuwaomba waendelee na moyo huo wa kusaidia watu wasiojiweza na wenye mahitaji
maalumu
No comments:
Post a Comment