Friday 10 February 2017

KUKOSEKANA KWA AFISA MTENDAJI KWAKWAMISHA MAENDELEO



Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi akizungumza na wananchi wa kijiji hicho

Kukosekana kwa  Afisa mtendaji zaidi ya  miaka Mitatu tangu mwaka 2014. kwenye kijiji cha Nyabalasana  Kata ya kakubilo kilichopo katika halmashauri ya Wilaya ya Geita, Jimbo la geita Vijijini  ni sababu ambayo imepelekea wananchi kushindwa kushiriki katika uchangiaji wa maendeleo  na kusababisha mapato mengi kupotea
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara Mahingu Masatu na Elias Nzobe wakazi wa kijiji hicho wametoa kero yao  mbele ya Mkuu wa wilaya ya Geita  ambapo wamemweleza kwamba kukosekana kwa mtendaji huyo ngazi ya kijiji imepelekea mapato mengi kupotea huku michango wanayochanga ikiwa haieleweki inafanya kazi gani na inakwenda wapi.

 
“ Kero ambayo imesababisha wananchi kugoma kuchangia madawati moja ni kutokana na watendaji wambao walikuwa wanakuja wanakusanya michango wanaondoka sasa tutaendelea paka lini unachanga kitu akifanyiki sisi tukaona ni bora kugoma”Alisema Maningu

“Kiini ni kutokana na swala la ujenzi wa choo kutokukamilika wa shule ya msingi Nyabalasana baada ya wananchi kuchanga na kuona kuwa kazi ijafanyika inavyotakiwa ndio sababu ambayo imetupelekea kugoma”alisema Nzobe

Akisoma taarifa ya kijiji hicho  Kaimu Afisa mtendaji wa kijiji hicho  Freda Bosha amebainisha namna  ambavyo mapungufu yalivyo kutokana na kukosekana kwa afisa mtndaji huku akimwomba mkuu wa wilaya kupatikana kwa mtendaji kijiji hapo.
“Kukosekana kwa afisa mtendaji ni chanzo kikubwa cha mapato mengi kupotea bila ya utaratibu Mh,Mkuu wa wilaya tunaomba kupatiwa mtendaji katika kijiji ili aweze kusimamia shughuli za maendeleo kijijini hapa”alisema Bosha

Kufuatia hali hiyo iliyochangia hata uwajibikaji wa wananchi kuchangia upande wa Madawati kusuasua, Mkuu wa Wilaya Mwl. Herman Kapufi pamoja na kuwahimiza  wakazi wa  Nyabalasana kuendelea kujitolea katika miradi ya maendeleo amewahakikishia kwa muda wa wiki mbili watampata afisa mtendaji, huku akimwachia jukumu hilo Afisa utumishi.

“Lakini msiwe na tabia ya kuzira kwasababu ya mtu fulani kama kuna tatizo mnakaa kwenye kikao  mnajadili mnatafuta mwafaka mwenyekiti inaonekana kuwa amezidiwa kutokana na kwamba akuna mtendaji wa kijiji  maana mtendandaji wa kijiji ndie mshauri bahati nzuri afisa utumishi yupo hapa naamini hatalifanyia kazi kwani ndie mwenye uwezo wa kuhamisha mtumishi”Alisema Kapufi

Katika hatua nyingine wakazi hao wakaliomba Shirika la Umeme Tanzania {TANESCO} Mkoa wa Geita kupitia mradi wa Umeme Vijijini REA  kuwafikishia nishati hiyo.

 Meneja wa Tanesco Mkoa wa Geita Joachim Ruweta akajibu maombi ya wananchi amesema,  serikali inampango wa kufikisha umeme katika vijiji vyote vya Mkoa huo, ambavyo havikufikiwa kupitia mradi huo mkubwa wa REA awamu ya pili.


“Wananchi wanatakiwa kuchangia kwa kuachia maeneo yao wazi ili waweze kusababisha huduma kufika kwenye maeneo ya makazi yao tunaendelea na jitihada za kusambaza umeme kwa awamu ya pili maeneo ambayo bado umeme ujafika”Alisema Ruweta

No comments:

Post a Comment