Wednesday 8 February 2017

MTOTO AFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA KATIKA BWAWA LA MAJI MKOANI GEITA



Mtoto mmoja amefariki dunia baada ya kuzama katika bwawa  la maji lililopo mtaa wa njia panda katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro wilayani na mkoani geita.
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na moja jioni ambapo mtu  huyo alikuwa akioga katika bwawa hilo akiwa na wenzake baada ya mda mfupi alipotea ghafla kutokana na bwawa hilo kuwa na kina kirefu ndipo  baadhi ya wakazi katika eneo hilo walipo  jitokeza na kujaribu kumtafuta ndani ya bwawa hilo lakini hawakufanikiwa kumuona , ndipo shughuli za kumtafuta mtu huyo zimeendelea tena  mapema hii leo na mnamo majira ya saa sita mchana  mwili wa marehemu huyo umefanikiwa kuonekana .

Akizungumza  Mwenyekiti wa mtaa huo Bw. Michael Chuma amemtaja aliyefariki dunia kuwa ni Kamugisha Budodi mwenye umri wa miaka 14 mkazi wa kijiji cha mapinduzi wilayani chato na alikuwa mwanafunzi  wa darasa la tano katika shule ya msingi mapinduzi .

Aidha  amewata  wazazi na walezi katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro  kutowaruhusu watoto wenye  umri  mdogo  kuchota maji wala kuoga  katika eneo hilo kutokana na bwawa hilo kuwa na kina kirefu pamoja na toze nzito kitu ambacho kina kuwa hatarishi kwa watoto hao.


Kwa upande wa  baadhi ya wakazi katika eneo hilo wameiomba Serikali ya mtaa huo kuweka uzio katika eneo hilo kwa lengo la kuzuia watoto wenye umri mdogo  kuto tumia bwawa hilo.

No comments:

Post a Comment