Monday 27 February 2017

WAKAZI WA KATA YA BUSERESERE MKOANI GEITA WAIOMBA SERIKALI KUBORESHA MIUNDOMBINU



Wakazi katika Kata ya Buseresere wilayani Chato  mkoani Geita wameiomba Serikali kuwaboreshea miundombinu ikiwa ni pamoja na mitalo ya kusafirisha maji taka ili kuepuka kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na mvua za masika kuanza kunyesha.
Hatua hiyo imekuja baada ya mvua za masika kuanza kunyesha kwa kasi katika eneo hilo jambo ambalo limesababisha maji kutuama katika makazi ya watu kutokana na ujenzi holela huku watoto wadogo wakihofiwa kufa maji kutokana na maji hayo  kutuama katika  mshimo ya taka yaliyopo  karibu na makazi ya watu.

Wakizungumza na Storm habari mapema hii leo kijijini hapo baadhi ya wakazi katika eneo hilo wamesema kuwa wanaiomba serikali kuwaboreshea miundo mbinu itakayo wezesha maji kuto tuama katika makazi ya watu kwani hali hiyo inakwamisha shughuli za kiuchumi kutofanyika hasa vyumba vya kulala wageni kukosa wateja kutokana na kujaa maji.

Kwa upande wake Mzee Shaaban Abeid ambae ni mwenyeji wa eneo hilo na aliwahi kuwa Afisa mtendaji wa kata ya Buseresere amesema kuwa madhara ambayo yanaweza kujtokeza kutokana na maji kukosa njia ya kupitia ni pamoja na nyumba zao kubomoka hasa kwa mvua zinazo nyesha nyakati za usiku.


Aidha Afisa mtendaji wa kijiji cha Buseresere Bw. Issa Mohamed Husein amesema kuwa kumekuwa na idadi kubwa ya nyumba ambazo zime jengwa kiholela katika eneo hilo na ameiomba serikali  kupitia halmashauri ya wilaya ya chato kuboresha miundombinu ikiwa ni pamoja na kupanga kijiji hicho ili kuondokana na  adha kama hizo.

No comments:

Post a Comment