Thursday 2 February 2017

IDARA YA UHAMIAJI MKOANI GEITA YAPEWA MAAGIZO



Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi.
Idara  ya uhamiaji  mkoani geita imewaomba wamiliki na wafanyakazi   wote  katika hotel  za  kitalii na nyumba za  kulala  wageni  kutoa ushirikiano kwa kuwapa taarifa pindi wanapokuwa na mashaka kwa raia yeyote ambaye anatoka nje ya nchi.

Akizungumza kwenye Semina ya kuwajengea uwezo na mbinu za kuwabaini  Raia wa kigeni   wanaoingia  nchini bila ya kuwa na utaratibu afisa uhamiaji mkoani geita Wilfred  Marwa amesema kuwa  wageni  wengi ambao wamekuwa  wakija wamekuwa wakifika kwenye hotel na kuendelea kufanya mambo ambayo  sio mazuri  katika  mkoa wa Geita.

Akifungua semina hiyo ya siku moja mkuu wa wilaya ya Geita mwl. Herman Kapufi amesema  kuwa  kuna imani ambayo imejengeka kwa wafanyabiashara  kuwa kwa mtu ambaye anakuwa na biashara nzuri na wateja wengi  kuhisiwa kuwa anatumia  dawa za kuvuta watu  jambo   ambalo ameeleza  ni imani potofu.


Kwa upande wao washiriki kwenye  semina  hiyo wameitaka  idara  ya uhamiaji kuwa na maadili yaliyo mema ikiwa ni pamoja na kutoa  vitambulisho pindi wanapokuwa kwenye zoezi la ukaguzi lakini pia kutunza siri kwani wengi wao wamekuwa wakiogopa kutoa   ushirikiano  kwa kuhofia  swala la usalama wao.

No comments:

Post a Comment