Friday 17 February 2017

WAKAZI WA GEITA WAMEIOMBA SERIKALI KUTATUA SUALA LA UHABA WA VITUO VYA AFYA




Wakazi wa Geita wameiomba Serikali kutatua  suala la uhaba wa vituo vya afya pamoja na zahanati mkoani hapa  kutokana  na  jambo  hilo kupigiwa kelele kila kukicha lakini limeonekana kuwa kama tatizo  la kudumu  kwa baadhi ya maeneo mkoani hapa.
Wakizungumza baadhi ya wananchi mkoani hapa wameiomba Serikali kusogeza  huduma hiyo katika mazingira husika ili kuepuka  msongamano  uliokithiri  katika  hospital teule ya  mkoa wa geita pamoja na kupunguza   vifo  visivyo  kuwa vya lazima kwasababu ya ukosefu wa vituo vya afya na zahanati vijijini .

Kwa upande wake Katibu wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ally Rajabu  amesema kuwa serikali inawajibu wa kushughulikia suala hilo kikamilifu, kama imeweza kupiga kampeni ya madawati kwa kila kijiji na imefanikiwa kwa asilimia kubwa  basi hata katika sekta ya afya inaweza  kufanya hivyo ili  kupunguza changamoto zinazo kabiri sekta hiyo.

Hata hivyo Kata ya Buhalahala ni miongoni mwa  kata iliyopo  katika halma shauri ya mji wa Geita na ina idadi kubwa ya wakazi lakini haina kituo cha afya wala zahanati jambo ambalo linawafanya wakazi wa eneo hilo kutembea kwa umbali mrefu kufika katika hospitali teule ya mkoa ili kupata huduma.


Kwa upande wa Diwani wa eneo hilo Bw.Eliasi Mussa  ambapo yeye amewataka wakazi katika kata hiyo kuwa wavumilivu kwani  suala hilo  la ujenzi wa kituo cha afya liko mbioni kukamilika  kwani kwa sasa  wanatafuta eneo ambalo lipo karibu na mazingira ya watu ili kujenga  ktuo cha afya  kwa lengo la kuondoa  adha inayo wasumbua wananchi katika eneo hilo.

No comments:

Post a Comment