Monday, 30 April 2018

MKUU WA JESHI LA POLISI NCHINI IGP SIMON SIRRO AMEFANYA UKAGUZI WILAYANI MUFINDI


Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akiwa ameongozana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, mhe. Jamhuri William (kushoto) wakati alipofanya ziara ya kikazi na kuzungumza na maofisa na Askari wa Jeshi hilo mkoani Iringa leo

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akisalimiana na Maofisa wa Polisi wakati alipofanya Ziara ya ukaguzi na kuzungumza na Maofisa na askari wa Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo. 


Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro, akizungumza na Askari wa Vyeo mbalimbali Wilayani Mufindi mkoani Iringa leo, wakati akiwa kwenye Ziara ya ukaguzi pamoja na kuona changamoto walizonazo Askari wa Jeshi hilo na kuwataka kufanyakazi  kuzingatia Sheria na Taratibu.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA KIKAO CHA KAZI MKOANI DODOMA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akifungua Kikao cha Kazi cha Mawaziri, Naibu Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Makatibu Wakuu, Wakuu wa Taasisi na Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hazina jijini Dodoma Jana Aprili 29, 2018.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

PICHA MATUKIO MBALIMBALI LEO BUNGENI MJINI DODOMA TAREHE 30 APRILI 2018


Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akiwasilisha  hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Fedha  kwa Wizara hiyo kwa mwaka 2018/19  Bungeni mjini Dodoma mapema leo. 


 Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Subira Mgalu akitoa maelezo Bungeni  mapema leo kuhusu mikakati ya Serikali kuhusu kufikisha umeme katika vijiji vyote hapa nchini.

 
Mbunge wa Mwanga Prof. Jumanne Maghembe akichangia hoja ya  Bajeti ya Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kuhusu mikakati inayoweza kusaidia kuendelea kukuza kiwango cha elimu hapa nchini.

  
Naibu Waziri wa  Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Elias Kuandikwa akijibu swali Bungeni  mjini Dodoma kuhusu hatua zinazochukuliwa na Serikali katika kujenga miundo mbinu  hapa nchini.


 Wageni mbalimbali walihudhuria Bunge wakiwemo Skauti  wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu mapema leo Bungeni mjini Dodoma.


Naibu  Waziri wa Fedha Dkt. Ashatu Kijaji akisisitiza jambo kwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhandisi Isack Kamwelwe leo mjini Dodoma. 

(Picha zote na MAELEZO)

NAIBU WAZIRI WA AFYA DKT. NDUGULILE AZINDUA BODI MPYA YA USHAURI WA HOSPITALI ZA WATU BINAFSI


Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile  akizindua Mwongozo wa viwango vya Msingi kwa vituo vya kutolea huduma za Afya katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.Kushoto kwake ni Msajili wa Hospitali Binafsi Dkt. Pamela Sawa.


 Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizindua kanuni za sheria ya uongozi wa hospitali za watu binafsi katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara hiyo Dk Otilia Gowele na Kulia ni Msajili wa Hospitali Binafsi Dkt. Pamela Sawa.


 Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizindua Mwongozo wa viwango vya Msingi kwa vituo vya kutolea huduma za Afya katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara hiyo Dk Otilia Gowele na Kulia ni Msajili wa Hospitali Binafsi Dkt. Pamela Sawa.

 
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akimkabidhi cheti cha shukrani kwa aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali za watu  binafsi Dkt.Mohamed Ally Mohamed katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.

  
Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa bodi mpya ya ushauri wa hospitali za watu binafsi mara baada ya kuizindua leo katika ukumbi wa LAPF leo Jijini Dodoma.

(Picha zote na Daudi Manongi MAELEZO-DODOMA)

Sunday, 29 April 2018

BINTI WA MIAKA 16 ALAZIMISHWA KUOZWA NA BABA YAKE MZAZI


Mtuhumiwa Bw. Saayai Petro ambaye anashitakiwa kwa kumuoa Binti wa miaka 16 akiwa amekamatwa


Mzee Kashirima Kashimba ambaye ni Baba wa Binti huyo akiwa amekamatwa baada ya kuwakimbia askari.


Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo akielezea hatua za kushikiliwa mzazi wa Binti huyo na dada yake na mwanaume ambaye alikuwa amemuoa.



Ikiwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inasisitiza wanafunzi kupelekwa shule na kupatiwa Elimu Bure Hali imekuwa ni Tofauti kwa  Binti mwenye umri wa miaka 16  ambaye anatoka Kata ya Kanyara Wilayani Geita amejikuta akilazimishwa kuozeshwa na mzazi wake wa kiume baada ya kumaliza darasa la saba na kufaulu kuendelea na masomo ya kidato cha  kwanza kwenye shule ya sekondari ya Kasamwa.

Friday, 27 April 2018

MBUNGE WA GEITA VIJIJINI JOSEPH MSUKUMA AWAKINGIA KIFUA WASANII BUNGENI


Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma amesema kufungia nyimbo za wasanii Nchini si jambo sahihi kwa Maendeleo ya Wasanii hao.

WANANCHI MKOANI GEITA WAPEWA ELIMU YA KUJIKINGA DHIDI YA UGONJWA WA MALARIA


Moja kati ya mwananchi (hayupo kwenye picha) akipima maralia kwenye viwanja vya Nyankumbu Mjini Geita.


Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akiwakabidhi baadhi ya akina mama vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu vinavyotolewa bure na serikali kwa wananchi.


Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kwenye maadhimisho hayo.


Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita akiwasilisha salamu zake kwenye maadhimisho hayo.




Ikiwa ni siku mbili zimepita  tangu kuadhimisha siku ya Malaria Mkoa wa Geita maambukizi ya ugonjwa huo yameshuka   kutoka asilimia 38.1 mwaka 2015/17 hadi asilimia 17 mwaka 2017/18 kwa mjibu wa takwimu za Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS).

RAIS MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA DODOMA-BABATI ILIYOKAMILIKA KUJENGWA KATIKA KIWANGO CHA LAMI

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe pamoja na  Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina, Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 iliyokamilika kujengwa katika kiwango cha lami, Kondoa mkoani Dodoma. Wengine katika picha ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli , Spika wa Bunge Job Ndugai, Wabunge pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amewashika mikono na kuwanyanyua juu, Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida  mara baada ya wote kwa pamoja kukata utepe kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.

  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akivuta utepe pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina kushoto na  Balozi wa Japan hapa nchini Masaharu Yoshida pamoja na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Pro. Makame Mbarawa kuashiria ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Chemba Juma Nkamia mara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma

  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina mara baada ya kufungua barabara ya Dodoma-Babati km 251 katika sherehe zilizofanyika Bicha Kondoa mkoani Dodoma  

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliojipanga kando kando ya barabara ya Dodoma-Babati mara baada ya kuifungua barabara hiyo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina wakati wa sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati Km 251

 
Kikundi cha kwaya cha JKT Makutupora kikitumbuiza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati km 251 zilizofanyika Kondoa mkoani Dodoma.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wakati akiwasili Kondoa kwa ajili ya sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza katika sherehe za ufunguzi wa barabara ya Dodoma-Babati yenye Km 251, Kondoa mkoani Dodoma


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Babati Mjini Pauline Gekul ambaye alihudhuria  katika sherehe hizo za ufunguzi wa Barabara ya Dodoma-Babati km 251, Kondoa mkoani Dodoma 

PICHA: WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA WADAU WA SEKTA ZA WIZARA YA HABARI BUNGENI LEO


Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Habari mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.

 
Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Utamaduni mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.

 
Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Sanaa na Mitindo mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.

 
Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa Muziki mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.


Viongozi wa wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Dini mara baada ya Waziri Dkt. Harrison Mwakyembe  kuwasilisha bungeni hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo katika viwanja vya bunge leo Jijini Dodoma.