Thursday 12 April 2018

WAFANYABIASHARA WADOGO WAOMBA KUPATIWA ELIMU YA MLIPA KODI



Baadhi ya wafanyabiashara wadogo Mkoani Geita wameiomba mamlaka ya mapato nchini (TRA) kuendelea kutoa elimu ya mlipa kodi kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu hiyo hali ambayo  imeendelea kuwafanya  kushindwa kutambua maana harisi ya kulipia kodi.

Wakizungumza  na  storm habari  wafanyabiashara hao akiwemo Mashaka Maige. na Anastazia Charles wameiomba mamlaka ya mapato nchini TRA kuwatembelea na kuwapatia elimu  Kwani  wengi wao awana  mwamko wa kulipia kodi kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha na kwamba kufanya hivyo kutawasaidia kutambua umuhimu wa kulipa kodi kwenye mamlaka husika.

Aidha  afisa mwandamizi wa huduma ya elimu kwa Mlipa kodi  toka makao makuu ya TRA nchini Bw,Maternus Mallya amesema kuwa tayari wamekwisha kuanza kutoa elimu kwa baadhi ya maeneo na kwenye Wilaya zilizomo Mkoani humo,Huku Meneja wa TRA Mkoani Geita James Jilala akisisitiza zoezi la usajili wa Tin namba kwa wafanyabishara  na kwamba kupitia elimu itawasaidia watu kujua maana harisi ya ulipiaji wa kodi.

No comments:

Post a Comment