Monday 16 April 2018

GGM YATOA MSAADA KWA MATIBABU KWA WAGONJWA WA MIDOMO SUNGURA




Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa mara nyingine umefanya zoezi la kuwasaidia wakazi wa Geita wenye matatizo ya mdomo sungura na wenye uvimbe kwenda kufanyiwa upasuaji jijini mwanza katika Hospitali ya Sekoture ikiwa ni muendelezo wa kusaidia jamii inayowazunguka katika kuwapa huduma mbalimbali za kiafya wananchi

Zoezi la kuwasaidia  wenye midomo sungura hufanyika kwa mwaka mara mbili ambapo kwa mwezi huu wa nne jumla ya watu wazima pamoja na watoto 25 wamepata nafasi ya kwenda kutibiwa.

Akiwaaga baadhi ya wagonjwa ambao wanatarajia kwenda kufanyiwa upasuaji kwenye Hospitali ya Sekoture ililiyopo jijini Mwanza Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi amewataka watu wengine kuwa na upendo na umoja ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa mtu ambaye anatatizo hilo pindi anapoitajika.

Ni zaidi ya watu laki saba wamekwisha kutibiwa tangu zoezi lianze mwaka 2014 .

No comments:

Post a Comment