Thursday 12 April 2018

WENYEKITI WA KIJIJI AIKIMBIA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA AKIHOFIA KUKAMATWA





Katika hali hisiyo ya kawaida Mwenyekiti wa kijiji cha Kilombero 1  Kata  ya Rwamgasa Wilayani Geita amejikuta akisusia  kikao cha ndani kilichoitishwa na Mkuu wa wilaya hiyo ambacho kilikuwa  na lengo la  kuleta suluhu baada ya wananchi kudaiwa kufunga ofisi ya kijiji kwa kile kilichoelezwa kuwa kuna ubadhirifu wa fedha za wananchi ambazo zilitolewa na mwekezaji wa mgodi mdogo wa Bingwa 

Mwenyekiti huyo ambaye anatambulika kwa jina la  Mahano Bwitonde  ameshindwa  kufika kwenye kikao hicho kilichokuwa na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya  wilaya sababu ikiwa ni  kutokomea na sh. Milioni moja fedha iliyotolewa na mwekezaji kwa ajili ya kikao cha wajumbe wa serikali ya kijiji hicho.

 Imeelezwa kuwa  Mwenyekiti huyo akiwa na Mtendaji wake wa Kijiji Suzana Chelehani  walifika katika mgodi wa Bingwa unaomilikiwa na Mwekezaji Mwananyanzala Husseni wakiomba posho kwa ajili ya kikao cha kumjadili na kumkaribisha katika kijiji hicho kama mwekezaji wa madini ya dhahabu kama ambavyo wamebainisha wajumbe wa serikali ya Kijiji hicho

No comments:

Post a Comment