Thursday 8 September 2016

SERIKALI YASISITIZA UMUHIMU WA MUSWADA WA SHERIA YA UPATIKANAJI WA TAARIFA YA MWAKA 2016


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa Michezo akichangia hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya upatikanaji wa Taarifa ya mwaka 2016 ambapo alisema Muswada huu utasaidia kuongeza uwazi na uwajibikaji pia utasaidia kukuza tasnia ya habari nchini, Wakati wa Kikao cha 2 leo Bungeni Mjini Dodoma.


Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Watu wenye Ulemavu) akichangia akichangia hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya upatikanaji wa Taarifa ya mwaka 2016 ambapo alisema Muswada huu utasaidia kukidhi hitaji la kikatiba la watu kupata taarifa, Wakati wa Kikao cha 2 leo Bungeni Mjini Dodoma.



Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju akichangia hoja kuhusu Muswada wa Sheria ya upatikanaji wa Taarifa ya mwaka 2016 ambapo alisema na kusisitiza umuhimu wa muswada huu ikiwemo kuongeza wigo wa upatikanaji wa taarifa kwa waandishi wa habari.


Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akijibu hoja zilizotolewa na wabunge kuhusu Muswada wa Sheria ya upatikanaji wa Taarifa ya mwaka 2016 ambapo aliwataka wabunge kuacha kupotosha kuwa muswada huu utavibana vyombo vya habari na kuwataka kuusoma na kuuelewa muswada huo

No comments:

Post a Comment