Friday 20 April 2018

HALMASHAURI YA MJI WA GEITA YA VIFUNGA VIBANDA 50 VYA WAFANYABIASHARA


Baadhi ya vibanda vya wafanyabiashara wa stendi ya mabasi Mkoani Geita vikiwa vimefungwa Mamlaka ya halmashauri ya mji wa Geita kutokana na wafanyabiashara kushindwa kulipa kodi ya elfu therasini na kudai kodi ya elfu kumi kuwa hipo kwa mujibu wa katiba ambayo waliandikishana na halmashauri hiyo.




Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa Nje ya vibanda vyao baada ya kufungwa na Halmashauri ya Mji wa Geita.


Baadhi ya wafanyabiashara wakiwa wamekaa wakitafakari hatua ya kufungiwa kwa vibanda vyao hali iliyowapelekea kushindwa kuendelea na Biashara.


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Bugomola akizungumza na wafanyabiashara baada ya kufika na kujionea hali hiyo.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Mhandisi Modest Aporinaly akizungumza juu ya hatua ambayo imechukuliwa ya kuvifungia vibanda ambavyo avijalipa  kodi ya elfu therasini.


Mwanasheria  wa Halmashauri hiyo Bashiri Mhoja akizungumzia kifungu ambacho kinamhurusu mkurugenzi kuvifungia vibanda vya wafanyabiashara hao kutokana na kukiuka makubaliano. 
Zaidi ya vibanda  Hamsini (50)  vya Wafanyabiashara kwenye Stendi kuu ya Mkoa wa Geita vimefungwa kwa madai ya kukaidi  agizo la kulipa kodi iliyo pangwa na Halmashauri ya Mji wa huo.

Wakizungumza   kwa  nyakati tofauti baadhi ya wafanyabiashara hao Bi. Mwajuma Hassani  na Bw. Sadick Mbido  wameilalamikia Halmashauri ya mji wa Geita kwa kitendo cha kukiuka makubaliano ya mkataba kwani kwasasa walikuwa wanalipa kodi ya Tsh. elfu kumi (10,000)  kwa mwezi ambapo ilikuwa ni ya mkataba unaoisha mwaka 2020 na  kwamba  ni jambo lililowashangaza kutokana na kulazimishwa kulipia kiasi cha Tsh. Elfu thelathini (30,000).

Hata  hivyo  Mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Stendi hiyo, Bw. Hamis Ayaki  amesema kuwa kitendo ambacho kimefanyika ni ukiukwaji wa makubaliano na kipo kinyume na makubaliano  na kwamba ameelezea namna ambavyo mkataba ulikuwa ukisema.

Kwa upande wa Katibu wa Wafanyabiashara Bw. Isack Shoo ameiomba Serikali kuwasaidia kutokana na wao kuendelea kulipia mapato ya Serikali na kwamba wana familia ambazo zinawategemea hivyo kufanya hivyo ni sawa na kuwaonea na kuwanyima haki zao za msingi.

Akizungumza na Wafanyabiashara hao baada ya kufika na kujionea kufungwa kwa Shughuli zao Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Geita, Bw. Leornad Bugomola amewataka kuwa watulivu na kwamba suala lao litashughulikiwa kwa wakati na watarudi kuendelea na shughuli zao.

“Ndugu zangu kwanza niwashukuru maana mmekuwa watulivu mmenipigia simu nimekuja na ndio tunataka namna hii sio kujichukulia hatua mkononi mimi nawaomba muwe watulivu ikiwezekana niondoke na viongozi wenu hili tufuatilie suala hili na likikamilika watawaletea majibu” Alisema Bugomola.

Kutokana na malalamiko hayo   Mkurugenzi  mtendaji wa halmashauri ya mji wa Geita, Mhandisi Modest Aporinaly  alisema wameshakaa na wamiliki wa Vibanda na wakaelewana kuwa watalipa Tsh. Elfu thelathini  hivyo kitendo ambacho wanakiona ni ukiukwaji wa makubaliano baina ya wamiliki wa Vibanda   na Wapangaji.

Mwanasheria  wa Halmashauri hiyo Bashiri Mhoja amesema kuwa ndani ya mkataba kipengele  namba tatu (3)  kinamruhusu Mkurugenzi kufanya mabadiliko baada ya kipindi cha miaka mitatu kutokana na mfumuko wa Bei.



No comments:

Post a Comment