Tuesday 10 April 2018

SERIKALI YAJIKITA KUWALINDA WATOTO WA KIKE DHIDI YA SARATANI




Serikali imezindua utoaji chanjo ya kudhibiti saratani ya shingo ya kizazi kwa watoto wa kike wa umri kati ya miaka TISA (9) na miaka 14.

Akizungumza kwenye shughuli hiyo Makamu wa rais kwa upande wake amesema ni jambo jema kwa Taifa kuwa na wananchi wenye afya na kuwalinda watoto katika magonjwa hatarishi.  

Aidha Makamu wa Rais amewaagiza Waganga Wakuu na Wilaya kuandaa kambi za wazi angalau mara tatu kwa mwaka ili kutoa fursa kwa wanawake wengi zaidi kupima saratani ya matiti nay a mlango wa kizazi.

Makamu wa Rais amesema Utoaji wa Chanjo dhidi ya Saratani ya mlango wa kizazi pamoja na uchunguzi wa awali kwa pamoja vitasaidia kuwakinga mabinti na kubaini mapema ugonjwa wa saratani kwa wanawake na hivyo kuepusha maumivu makali ama vifo vinavyoweza kuzailika

Tunatakiwa hadi Desemba, 2018 tuwe tumewafikia wanawake milioni tatu. Hii itawezekana endapo kila mmoja wetu ataweka kipaumbele katika kufikia lengo hilo.” Amesisitiza Makamu wa Rais.

Makamu wa Rais amesema kuwa Serikali itatoa chanjo ya kuzuia saratani ya mlango wa kizazi bila malipo yoyote katika vituo vinavyotoa huduma za chanjo vya Serikali, Mashirika ya Dini na Taasisi Binafsi.

No comments:

Post a Comment