Friday 27 April 2018

MBUNGE WA GEITA VIJIJINI JOSEPH MSUKUMA AWAKINGIA KIFUA WASANII BUNGENI


Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma amesema kufungia nyimbo za wasanii Nchini si jambo sahihi kwa Maendeleo ya Wasanii hao.

Akizungumza katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Mwaka 2018/19, Msukuma amesema Wasanii nchini wanalenga Soko la kimataifa na kwamba haiwezekani wapeleke Video za nyimbo zao katika soko la kimataifa ikiwamo Marekani wakiwa wamerekodi huku wamevaa Madela.

Amesema ni jambo lisiloingia akilini watu kutazama video za mwanamuziki Rihanna katika vituo mbalimbali vya televisheni, huku wahusika wakiwa wamevaa nusu utupu, huku zile za Tanzania zikifungiwa.

“Mtu kaimba wimbo mwaka mzima uliopita leo waziri unaibuka na kufungia. Huko vijijini watu wameshaipata hizo nyimbo, mnatupa taabu sana huko vijijini maana watendaji wanakamata kompyuta za watu zenye nyimbo zilizofungiwa,” amesema Msukuma.

“Msitumie muda mwingi kufungia nyimbo, tumieni muda mwingi kuwaelimisha hawa wasanii maana wanatumia muda mrefu sana kutengeneza nyimbo zao.” Alimalizia kwa kusema hivyo

No comments:

Post a Comment