Wednesday 25 April 2018

WANAUME KATIKA MTAA WA BUYEGULE, NYANKUMBU WASUSIA KUCHIMBA KABURI NA KUWAACHIA WANAWAKE






Ukisitaajabu ya Mussa utayaona ya filauni, usemi huu umejidhihirisha katika Mtaa wa Buyegule kata ya Nyankumbu Halmashauri ya mji wa Geita baaada ya wanaume kugoma kushiriki Shughuli za uchimbaji wa kaburi  kutokana na kifo cha ghafla cha Mzee Kangeko Vigume mwenye umri wa miaka 57 na kuwataka wanawake washiriki shughuli hizo kwa madai kuwa   wamekuwa  chanzo cha vifo vya wanaume kwenye mtaa huo
Imezoeleka kuwa kwenye Jamii zetu wanaume ndio wanahusika kufanya Shughuli za Uchimbaji wa kaburi na kubeba mwili wa Marehemu lakini kwenye Mtaa huo hali imekuwa ni tofauti kutokana na madai ya wanaume kulalamika kuwa wameendelea kupoteza maisha kwenye Mazingira ya kutatanisha na kujikuta wakiendelea kuisha kufanya hivyo ni Adhabu tosha kwa wanawake ambao wamekuwa na tabia za kishirikina.


Wakizungumza kwa vipindi Tofauti na Storm  Habari kwenye familia ya mzee Kangeko Vigume ambaye amefariki kutokana na kuugua ghafla wamesema kuwa tukio hilo la kufa mwanaume ghafla sio la kwanza na kwamba hadi sasa kuna wanaume saba wamepoteza maisha kwenye Mazingira ya kutatanisha  na jambo ambalo limewashanga mahiti hiyo imekuwa ikigeuka pindi wanapohilaza


No comments:

Post a Comment