Monday 16 April 2018

MKOA WA GEITA WAZINDUA KAMPENI YA TAFAKARI YA ULINZI NA USALAMA




Serikali Mkoani Geita imewaonya watu au vikundi ambavyo vitaonekana kuvunja amani ya Mkoa  na kwamba mkoa upo imara katika kudumisha suala la ulinzi na usalama.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel wakati alipokuwa akizungumza na vikosi vya ulinzi na usalama nje ya ofisi za mkoa.

Amesema ni vyema kwa jamii  ikatambua   kuna walinzi hivyo wanawajibu wa kutii sheria  bila ya kushuru  kwenye maeneo ambayo wanaishi.

Aidha Mkuu wa mkoa Ameongeza kwa kusema anatambua changamoto walizonazo Askari katika utendaji wao wakazi hivyo ilikuwafanya wapate nguvu za kufanya kazi tayari wamekwisha kuanza mchakato wa ujenzi wa Nyumba 100.

Mkuu wa Mkoa amesema  kumekua na imani potofu za mauaji ya vikongwe, Maaskari na walinzi kwa imani ya kupata mali kupiti damu ya watu hao,hivyo ameagiza vikosi hivyo kupinga na kupambana vikali na vitaa hiyo ili kutokomeza mauwaji hayo.

Mkoa wa Geita Upo kwenye Kampeni ya Wiki mbili ambayo inaitwa TAFAKARI YA ULINZI NA USALAMA MKOA WA GEITAinayotarajia kumalizika  tarehe 28 ambayo inalengo la kudumisha amani ya Mkoa huo.

No comments:

Post a Comment