Thursday 26 April 2018

WATUMISHI 7 WAFUKUZWA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA


Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga akitangaza hatua zidi ya watumishi saba ambao wamekutwa na tuhumza za utoro kazini pamoja na wizi.


Baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita wakiwa kwenye kikao cha tatu cha baraza hilo.



Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel akielezea mikakati ya kuanzishwa miradi ambayo itaweza kuhisaidia halmashauri hiyo kuongeza vipato wakati alipozungumza kwenye baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Geita.



Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Geita imewafukuza kazi watumishi saba kutokana na kuwa na makosa   ya utoro kazini , Udanganyifu na wizi wa fedha na rasilimali za umma ikiwa ni pamoja na  Kushindwa kuwasilisha mapato ya serikali  na Kutokuwajibika.

Mamlaka ya Baraza la Madiwani imepewa nguvu ya kisheria kuwawajibisha watumishi wa Halmashauri isipokuwa walimu na wale wanaoteuliwa na Mhe. Rais au Waziri mwenye dhamana kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na.8 ya mwa ka 2002 kama ilivyofanyiwa marekebisho na Sheria Na.19 ya mwaka 2002, kifungu cha  6 (6).

Akitoa adhabu hiyo kwenye ukumbi wa Mikutano Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Elisha Lupuga amesema  Kwa mujibu wa kanuni ya 42(2) na kanuni ya 43(2) ya Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, aina ya makosa na adhabu zimeainishwa katika nyongeza Na.1 na nyongeza Na. 2. kwamba adhabu ambazo zimeainishwa ni pamoja na kufukuzwa kazi ,kupunguziwa mshahara au 
kushushwa cheo.

“Hivyo kamati imejiridhisha na kuona wanastahili adhabu ya kufukuzwa kazi kutokana na kukiukwa sheria ya ajira” Alisema Lupuga.

Mwenyekiti Lupuga amewataka watumishi ambao ni watoro na si waaminifu, waadilifu na  wezi na hawana nidhamu kwenye Utumishi wa Umma wajipange la sivyo hawatabakia kufanya kazi ndani ya Halmashauri ya hiyo kwani Hawatavumiliwa kutokana na vitendo hivyo.

Hata hivyo kwa upande wake Diwani wa Nyawilemelwa,Method Gaspeli amesema maamuzi ambayo yamechukuliwa na baraza hilo yako sawa kwani yatawasaidia watumishi wenye tabia za namna hiyo kujirekebisha.


Sanjali na hayo Mkuu wa Mkoa Huo Mhandisi Robert Gabriel amelitaka baraza hilo kuwa na mkakati wa kuainisha mradi kwa kila mwaka ambao utasaidia kuingiza mapato kwenye halmashauri hiyo.

No comments:

Post a Comment