Tuesday 17 April 2018

RAIA WA BURUNDI 30 WALIOKUWA WAKIISHI KINYUME CHA SHERIA WAKAMATWA MKOANI GEITA


Vijana therasini ambao ni Raia wa nchi ya Burundi wakiwa wameshikiliwa na Idara ya uhamiaji Mkoani Geita Kabla ya kufikishwa mahakamani.


Naibu kamishina wa idara ya uhamiaji Mkoani Geita, Wilfred Marwa  akizungumza na waandishi wa habari  ofisini kwake.


Idara ya uhamiaji Mkoani Geita imewakamata Raia wa Burundi Therasini (30) ambao wanaishi na kufanya kazi Nchini kinyume cha sheria na wengine wakikamatwa kwenye zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya Taifa ambalo linaendelea Mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za uhamiaji Mkoani humo, Naibu kamishina wa idara ya uhamiaji Mkoani Geita, Wilfred Marwa amesema  kati  ya hao Raia kumi na nane ( 18)  wapo nchini kinyume na sheria na wanafanya kazi mbalimbali za kujiingizia kipato na wengine  kumi na mbili (12) walikuwa kwenye zoezi la kujiandikisha vitambulisho vya Taifa jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Naibu kamishina Marwa ametaja kazi ambazo wamekuwa wakizifanya Raia hao wa kigeni kuwa ni kazi za kilimo na ufugaji.

“Mara nyingi watu hawa wanajishughulisha sanaa na kazi za  ufugaji wa Ng’ombe na kilimo cha 
Mananasi pamba na mpunga kwenye maeneo ya vijijini” Alisema Marwa.

Aidha kwa upande wake moja kati ya Raia wa Burundi aliyekamatwa na idara ya uhamiaji Bw,Kajoro Richard alisema sababu ambazo zimekuwa zikisababisha kuingia nchini ni kutokana na ugumu wa maisha nchini mwao na kukosekana kwa ajira.

“Mimi Kweli nilikuja hapa Tanzania nikitokea nchini kwetu Burundi kwa sababu ya kuja kutafuta maisha kwetu ajira ni ngumu sanaa ila naomba wanisamehe nipo tayari kurudi nchini kwetu”Alisema Kajoro.

Naibu kamishina Wilfred Marwa amesema zoezi hilo ni endelevu na kwamba amewataka raia wa kigeni kufuata utaratibu kwa kufuata vibari vya kukaa nchini kwa njia ya halali huku akiwataka watanzania ambao wanaishi na Raia hao kuachana na tabia hiyo na kwamba watakamatwa watafungwa kifungo cha miaka  20 au faini ya milioni ishirini 20.

No comments:

Post a Comment