Wednesday 25 April 2018

MWENYEKITI KIJIJI CHA MAPINDUZI MKOANI GEITA AHIMIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA




Mwenyekiti wa Kijiji cha Mapinduzi Wilayani Chato mkoani Geita Bw. Kitute Kalegea amesema hata mvumilia mtu atakaye shindwa kusafisha Mazingira kwa kufyeka nyasi na kufukia madimbwi ya maji kwa lengo la kuendelea kutokomeza mazalia ya mbu waenezao ugonjwa wa malaria.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Storm Habari kijijini humo ambapo amesema kuwa  ugonjwa wa Malaria katika kijiji hicho umeendelea kuwa tishio kutokana na baadhi ya wananchi kushindwa kuzingatia suala la usafi wa mazingira ikiwemo kuharibu mazalia ya mbu waenezao Ugonjwa huo.

Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ameahidi kuwachukulia hatua za kisheria baadhi ya watu wanaotumia vyandarua vya kujikinga na mbu kwa matumizi yasiyo sahihi ikiwemo kufugia kuku.
Aidha baadhi ya Wananchi katika Kijiji hicho wameiomba Serikali kuendelea kutoa Elimu ya matumizi sahihi ya Vyandarua hususani Vijijini ili kuendelea kupambana na kutokomeza maambukizi ya Ugonjwa huo.

No comments:

Post a Comment