Friday 27 April 2018

WANANCHI MKOANI GEITA WAPEWA ELIMU YA KUJIKINGA DHIDI YA UGONJWA WA MALARIA


Moja kati ya mwananchi (hayupo kwenye picha) akipima maralia kwenye viwanja vya Nyankumbu Mjini Geita.


Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akiwakabidhi baadhi ya akina mama vyandarua vyenye dawa ya kuua mbu vinavyotolewa bure na serikali kwa wananchi.


Mkuu wa Mkoa Geita, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kwenye maadhimisho hayo.


Mwakilishi wa Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji wa Geita akiwasilisha salamu zake kwenye maadhimisho hayo.




Ikiwa ni siku mbili zimepita  tangu kuadhimisha siku ya Malaria Mkoa wa Geita maambukizi ya ugonjwa huo yameshuka   kutoka asilimia 38.1 mwaka 2015/17 hadi asilimia 17 mwaka 2017/18 kwa mjibu wa takwimu za Tanzania Demographic and Health Survey (TDHS).
Aidha takwimu hizo kitaifa zinaonyesha kwamba maambukizi ya ugonjwa wa Malaria yameshuka kutoka wastani wa asilimia 14 mwaka 2015/16 hadi asilimia 7.3 mwaka 2017/18.

Akizungumza na wananchi kwenye viwanja vya Nyankumbu Mjini Geita wakati wa utoaji wa elimu  juu ya kujikinga na maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria Mkuu wa

Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel  amesema mafanikio hayo ni matokeo ya kazi nzuri ya serikali ya awamu ya tano ambayo imedhamiria kuondoa vifo vinavyotokana na Malaria ambapo takwimu zinaonyesha kwamba wastani wa mtu mmoja hupoteza maisha kila baada ya dakika moja kutokana na ugonjwa huo unaoambukizwa na mbu jike aina ya “Anopheles”.

Ameongeza kuwa  serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya inaendelea na mapambano dhidi ya Malaria ambapo mwaka jana ilitoa lita 8,380 za dawa ya viua dudu katika mazalia ya mbu pamoja na kugawa bure vyandarua vyenye dawa kwa wananchi.

Mganga Mkuu mkoani Geita, Dr.Japhet Simeo Amebainisha kwamba mkoa wa Geita unasumbuliwa na maambukizi ya Malaria kutokana na sababu za kimazingira ambapo kuna nyuzi joto 18 hadi 32 linalochochea uendelevu wa mbu hivyo ni vyema wananchi wakahakikisha wanatunza vyema mazingira yao ikiwemo kufyeka nyasi na kufukia madimbwi ili kuangamiza mazalia ya mbu.

Wananchi na wanafunzi mkoani Geita waliitikia vyema zoezi la upimaji Malaria na utoaji bure dawa kwa waliobainika kuwa na ugonjwa huo .



No comments:

Post a Comment