Tuesday 17 April 2018

WASICHANA WENYE UMRI WA MIAKA 14 KUPATIWA CHANJO YA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI GEITA


Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na wadau wa sekta ya afya awapo kwenye picha)juu ya zoezi la Chanjo kwa Mabinti wa miaka 14 Mkoani humo


Mratibu wa huduma za chanjo Mkoani Geita,Bi Wille Luhangija akitoa mafunzo ya namna ya kujikinga na saratani ya mlango wa Kizazi.


Wadau wa sekta ya afya wakifuatilia mafunzo ya chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi.


Mratibu msaidizi wa afya ya uzazi Mkoani Geita,Bi Mbeleje Donald akitoa maelekezo ya namna ambavyo watoa huduma wanatakiwa kuzingatia wakati wa zoezi la Chanjo ya mlango wa uzazi.


Mkoa wa Geita unatarajia kuanza zoezi la chanjo ya  kuzuia saratani ya mlango wa kizazi kwa Wasichana wenye Umri wa miaka kumi na nne(14) lengo likiwa ni kuwakinga na maambukizi ya virusi vya Human Papilloma.

Saratani ya Mlango wa kizazi imekuwa ikiongezeka kila mwaka kwa nchi  na takribani watu elfu hamsini wamekuwa wakiongezeka  na kusababisha vifo vya wakina mama wengi pamojana na mabinti.

Akizungumza na wadau wa sekta ya afya Mkoani hapa Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel ametaja sababu ambazo zimeendelea kusababisha Saratani ya mlango wa kizazi  ni pamoja na kujamiiana kwenye umri mdogo, kuwa na wapenzi wengi, ndoa za mitaara pamoja na uvutaji wa sigara.

“Ndugu washiriki  kuna dalili ambazo zinaweza kusababisha ugonjwa wa saratani Kuto kwa damu bila mpangilio au kutokwa damu baada ya kujamiana Maumivu ya mgongo, miguu na au kiuno Kuchoka, kupungua uzito, kupungikiwa hamu ya kula Kutokwa uchafu uchafu kwenye uke wa majimaji, uliopauka wa rangi kahawia au wenye damu Kuvimba mguu mmoja” Alisema Robert.

Kwa upande wake Mratibu msaidizi wa Afya ya uzazi Mkoani humo,Bi Mbeleje Dornad alisema kwa hapa nchini takribani wanawake laki nne na sitini na tisa elfu wamegundulika na maambukizi ya saratani ya mlango wa kizazi.

Inakadiriwa kuwa kila mwaka kati ya wanawake 466,000 wanathibitika kuwa na saratani ya mlango wa kizazi, na  wengi wao wako katika nchi zinazoendelea” Alisema Bi,Mbeleje.

Kaimu Mganga mganga Mkuu wa Mkoa wa Geita,Joseph Odero amewataka wazazi pamoja na walenzi kutoa ushirikiano pindi zoezi hilo litakapo anza tarehe 23 mwezi huu wa aprili hikiwa ni pamoja na kuwaruhusu mabinti wenye umri wa miaka 14 kufanyiwa chanjo hiyo.

Takwimu kutoka hospitali ya Occean Road inaonyesha kwamba, Saratani ya Mlango wa Kizai inachangia kwa asimilia 36 ya saratani zote, Asilimia 70 ya wagonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi wanajitokeza katika hatua ambayo tayari saratani imesha samba maeneo mengine mwilini.


No comments:

Post a Comment