Sunday 29 April 2018

BINTI WA MIAKA 16 ALAZIMISHWA KUOZWA NA BABA YAKE MZAZI


Mtuhumiwa Bw. Saayai Petro ambaye anashitakiwa kwa kumuoa Binti wa miaka 16 akiwa amekamatwa


Mzee Kashirima Kashimba ambaye ni Baba wa Binti huyo akiwa amekamatwa baada ya kuwakimbia askari.


Kamanda wa Polisi Mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo akielezea hatua za kushikiliwa mzazi wa Binti huyo na dada yake na mwanaume ambaye alikuwa amemuoa.



Ikiwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  inasisitiza wanafunzi kupelekwa shule na kupatiwa Elimu Bure Hali imekuwa ni Tofauti kwa  Binti mwenye umri wa miaka 16  ambaye anatoka Kata ya Kanyara Wilayani Geita amejikuta akilazimishwa kuozeshwa na mzazi wake wa kiume baada ya kumaliza darasa la saba na kufaulu kuendelea na masomo ya kidato cha  kwanza kwenye shule ya sekondari ya Kasamwa.
Binti huyo Alifaulu mwaka 2017 kuingia kidato cha kwanza mwaka 2018 katika shule ya sekondari Kasamwa lakini hakuwahi kuhudhuria masomo hata siku moja.

Baba mzazi aliyejulikana kwa jina la Kashirimu Mashimba amepokea posa ya Ng’ombe watano kutoka kwa Saayai Petro aliyetaka kumuoa binti mwenye umri wa miaka 16.

Kaimu afisa mtendaji wa Kata ya Kanyara Bw,Augustino Kazanza amesema kuwa walibaini kuwa binti huyo amehozeshwa kutokana na kupata taarifa kwa wananchi wenye mapenzi mema.

Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Mhanidisi Modest Aporinaly amesema kuwa bado kuna changamoto ambazo zimeendelea kujitokeza kwa watoto wa kike kupata mimba wakiwa shuleni kutokana na baadhi ya watu kuendelea kuendekeza mali na kuacha kuwapa Elimu wasichana.

Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi amelaani kitendo hicho na kuwataka wananchi kuwa mstari wa mbele kutoa taarifa dhidi ya watu ambao wanawahozesha wanafunzi

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema hadi sasa wanawashikilia watu watatu ambao ni Dada,Baba pamoja na kijana ambaye ndiye muoaji


Ikumbukwe tu kuwa Mkoa wa Geita katika takwimu za wanafunzi watoro inashika nafasi ya Pili kwa Skondari asilimia 8.1 na msingi asilimia 3.1

No comments:

Post a Comment