Monday 23 April 2018

MVUA ZINAZOENDELEA NCHINI ZAUA WATU 7 MKOANI GEITA



Baadhi ya makazi ya watu yakiwa yamejaa maji kwenye mitaa ya Mwatulelo Kata ya Buhalahala Mjini Geita kutokana na mvua ambazo zinaendelea Kunyesha.


Wananchi wakipita kwa shida kwenye barabara za mitaa ya Mwatulelo kutokana na mvua ambazo zinaendelea Kunyesha Mkoani Geita.


Nyumba ikiwa imeezuliwa paa  na kuanguka kutokana na mvua ambazo zinaendelea kunyesha Mkoani Geita.
Mvua  zinazoendelea Kunyesha Mkoani Geita zimesababisha  maafa ya vifo vya  watu saba   (7) watano wakitokea kwenye halmashauri ya wilaya ya Nyang’wale na wawili kwenye halmashauri ya Mji wa Geita.


Watu hao wamefariki kutokana  kujaa maji  mto ambao upo kwenye mpaka wa Wilaya ya Nyang’whale   na Sengerema huku mtu mmoja akiagukiwa na ukuta wa Nyumba na mwingine akifariki kutokana na kusombwa  na maji .

Akizungumza kwa njia ya Simu na  mtandao huu Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale Hamim Gweyama amesema  hadi sasa mwili ambao umetambuliwa  na ndugu ni mmoja na kwamba wanaendelea na jitihada za kutafuta miili mingine kwenye Mto huo.

Aidha kwa upande wake Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la zima Moto na uwokoaji Mkoani Humo Stanley Paschal  akizungumza na waandishi wa habari amesema watu hao wawili miongoni mwao ni mtoto mwenye umri wa miaka minne ambaye anajulikana kwa jina la Aneth Juma na Mzee Vicent Kipili ambaye aliangukiwa na ukuta ,huku akiwataka wananchi kuwa waangalizi wa watoto wao kwenye kipindi hiki cha msimu wa mvua.

Kwa upande wa Mashuhuda wa ajali ya Mtoto huyo Bi. SCOLA SANGA NA LUNYIRI  TEKANISA ambao ni wakazi wa Mtaa wa Kivukoni Kata ya Nyankumbu wamesema kuwa walimuona mtoto huyo akielea kwenye mtaro ndipo walipochukua jukumu la kumsaidia kumtoa na walipomtoa walimkuta amekwisha kufariki.

Ikumbukwe kuwa mamlaka ya hali ya hewa hivi karibuni imetaja mikoa ambayo itapata mvua kwa wingi ikiwemo na Mkoa wa Geita na kuwataka wananchi ambao wanaishi kwenye maeneo ya mabonde kuchukua taadhari mapema kwani mvua hizo zitaendelea hadi mwezi wa tano.

No comments:

Post a Comment