Mkuu wa mkoa wa Geita Meja
Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga
amesema kuwa miradi mbalimbali
inayoanzishwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), bado haieleweki kwa Wananchi hali
ambayo inasababisha kuwepo kwa malalamiko mengi.
KUHABARISHA NA KUFAHAMISHA KUHUSU HABARI NA MAMBO YANAYOENDELEA KATIKA JAMII YA GEITA, KANDA YA ZIWA, TAIFA NA DUNIANI. TUTUMIE HABARI AU WASILIANA NASI KUPITIA info@stormfm.co.tz au +255 685 883 870
Tuesday, 31 May 2016
SERIKALI KUANZISHA BENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia na Waziri wa Nishati
na Madini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa
Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda ya
bidhaa zinazotoka viwandani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa
wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiongea na wadau wa sekta ya
Viwanda wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa
Viwandani kwa mwaka 2015 na kuwataka kuunganisha nguvu katika uanzishaji na
uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali
itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo ya shirikisho la
viwanda nchini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa
Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI)
Leodger Tenga na wa pili ni Mwenyekiti wa Shirikisho la
Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe.
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wadau wa sekta ya
viwanda nchini(hawapo pichani) na kuwaahidi kuwaunga mkono katika harakati za
kuendeleza sekta ya viwanda ikiwamo kuanzisha banki ya maendeleo ya viwanda
nchini itakayosaidia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wale wenye nia ya
kuanzisha viwanda.
Wadau wa Sekta ya
Viwanda nchini wakimsilkiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa
Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa washindi wa
tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es
Salaam.
Monday, 30 May 2016
WABUNGE 7 WA UPINZANI WASIMAMISHWA KUHUDHURIA BUNGENI
Akisoma maamuzi hayo ya Bunge Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika amesema Januari
27.01.2016 wabunge hao walikiuka sheria na taratibu za kuongoza bunge kwa
walishinikiza kiti cha spika kijadili hoja ambayo ilikwisha tolewa uamuzi na
kiti hicho.
WANANCHI MKOANI GEITA WALALAMIKIA KUTOZWA PESA ZA KUANDIKISHWA KATIKA DAFTARI LA MAKAZI
Wakazi wa
mtaa wa
Uwanja kata ya Nyankumbu mkoani Geita
wamelalamikia suala la kutozwa pesa kwa ajili ya kuandikishwa katika daftari
linalowatambulisha kuwa ni wakazi wa eneo hilo pindi wanapohamia katika
mtaa huo.
Saturday, 28 May 2016
KUELEKEA FAINALI YA UEFA, FAHAMU MAMBO 14 MUHIMU KATI YA SIMEONE NA ZIDANE

Kesho Mei 28
katika dimba la San Siro, kutakuwa na pambano kali la fainali ya UEFA pale Real
Madrid watakapokuwa wakichuana na mahasimu wao wakubwa Atletico Madrid. Hii
imekuwa ni fursa adhimu sana kwa makocha wa timu zote mbili yaani Zinedine
Zidane na Diego Simeone kuoneshana umwamba kutokana na wote kuwa na historia ya
kuvichezea vilabu hivyo.
REKODI YA SERENGETI INDIA YAWAPAGAWISHA WAKENYA.
Kikosi cha timu ya soka ya Serengeti Boys.
Serengeti Boys imecheza mfululizo
michezo 7 ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Kore, Malaysia,
na Marekani (USA).
ULIMWENGU NAYE KUIKOSA STARS DHIDI YA HARAMBEE KESHO
![]() |
Mchezaji Thomas Ulimwengu |
Mchezo wa kirafiki wa kimataifa
kati ya wenyeji Kenya na Tanzania, Taifa Stars utapigwa kesho katika Uwanja wa
Moi Kasarani mjini Nairobi, Kenya kuanzia Saa 10:00 jioni.
Thursday, 26 May 2016
TAIFA STARS KUCHEZA NA HARAMBEE BILA SAMATTA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta(pichani
kushoto) hataweza kusafiri na Taifa Stars kwenda
Nairobi, Kenya kucheza na wenyeji Harambee Stars mchezo wa
kirafiki wa
kimataifa.
KRC Genk imemuombea Samatta kutorejea nchini kwa ajili ya mchezo
huo kwa sababu inamuhitaji katika mechi ya mchujo wa mwisho wa kuwania tiketi
ya kucheza michuano ya Europa League.
Na kwa ombi hilo la timu hiyo ya Ubelgiji, Samatta hatakuwemo kwenye msafara wa unaoondoka kesho saa 12.00 Alfajiri chini ya makocha wake, Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco.
Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.
Na kwa ombi hilo la timu hiyo ya Ubelgiji, Samatta hatakuwemo kwenye msafara wa unaoondoka kesho saa 12.00 Alfajiri chini ya makocha wake, Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco.
Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.
Wednesday, 25 May 2016
RAIS MAGUFULI AMTEUA WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU HURIA (OUT)
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu
Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania
(OUT).
Mheshimiwa Mizengo
Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti
Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.
Taarifa iliyotolewa
leo tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza
kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Mei, 2016
SERIKALI YAWEZESHA VIKUNDI 1,200 VYA WAKULIMA KUPATA MASOKO
Serikali imefanikiwa kuwezesha vikundi 1200 vya wakulima wadogo
wadogo nchini ili kupata masoko ya uhakika ya mazao yao wanayozalisha.
USAJILI WA WAFANYAKAZI WA UMWAGILIAJI DAWA ZA UKOKO WAINGIA DOSARI MKOANI GEITA
Wananchi mkoani Geita wamelalamikia kuwepo kwa tabia ya
kuchukuliwa watu wa mikoa ya nje katika
zoezi la usajili wa wafanyakazi wa umwagiliaji dawa za viuatilifu vya mbua.
HUYU NDIYE NYOTA ALIYEAPA KUFIA MSIMBAZI LICHA YA KUTAKIWA JANGWANI

Beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein Tshabalala, amesikia kwamba Yanga wanaitaka saini yake kwa udi na uvumba na alichowaambia ni kwamba wasahau mpango huo.
SERENGETI BOYS YAITUNGUA MALAYSIA 3-0 NA KUSHIKA NAFASI YA TATU.

Serengeti Boys wameibuka na ushindi wa
mabao 3-0 dhidi ya Malaysia katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu katika
michuano ya vijana ya AIFF ya nchini India.
TANESCO YAWATAKA WATEJA WAKE KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI ZA MATUMIZI YA UMEME
Meneja wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi Kutoka
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Majige Mabula akiongea na
waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo aliwataka wateja wa shirika hilo
kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme ili kuepuka ajali zinazoweza
kusababishwa na hitilafu za umeme.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bw.
Yasini Silayo.
Tuesday, 24 May 2016
SERIKALI IMEDHAMIRIA KUIFANYA TANZANIA KUWA NCHI YENYE UCHUMI WA KATI KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis
Mwinyimvua(Kushoto) akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa wadau wa
biashara nchini uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara
katikati ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania
Godfrey Simbeye na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi.
CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA(CBE) CHAWATAKA WANANCHI KUPUUZA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZINAZOTOLEWA NA VYOMBO VYA HABARI
Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emmanuel Mjema akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) inayoonesha kuwa chuo hicho kimepata ziada ya bilioni 1.2 kati ya mwaka huu na kufanya chuo kujiendesha kwa faida tofauti na baadhi taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari.
YANGA KUKUTANA USO KWA USO NA TP MAZEMBE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

Droo ya kupanga makundi mawili ya timu zitakazo
cheza katika kuwania nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la
shirikisho Afrika imetoka ambapo timu ya Tanzania bara klabu ya Yanga ipo Group A
itapambana na timu za TP Mazembe (Congo DR), MO Bejaia (Ageria) na Medeama
(Ghana).
VITA YA AZAM FC NA YANGA SC KOMBE LA SHIRIKISHO KUJULIKANA KESHO
Mchezo huo utapigwa kesho kuanzia saa 10:30 jioni kwenye
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam huku waamuzi wasaidizi watakuwa Ferdinand
Chancha wa Mwanza (line 1) na upande wa pili ni Soud Lila wa Dar es Salaam
(line 2) na mwamuzi wa akiba ni Frank Komba wa Dar es Salaam pia na Kamishna wa
mchezo huo atakuwa Juma Mgunda wa Tanga.
Monday, 23 May 2016
MANCHESTER UNITED YAMFUTA KAZI LOUIS VAN GAAL
Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amefutwa
kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester United ,huku aliyekuwa mkufunzi wa
Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua mahala pake.Raia huyo wa Uholanzi
anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya
mitatu.Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliripoti siku ya Jumamosi
kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi
yake ya mwisho akiwa mkufunzi.Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa
baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu
wa United siku ya Jumanne.
JUMA ABDUL NDIYO MWANASOKA BORA WA MWEZI APRIL

Beki wa kulia wa timu
ya soka ya Young African ya Dar es Salaam, Juma Abdul ameteuliwa kuwa mchezaji
bora wa mwezi Aprili, 2016 baada ya kura zake kuwashinda Donald Ngoma ambaye
pia anakipiga Young Africans na Hassan Dilunga wa JKT Ruvu ya Pwani.
SPIKA ASEMA BAADHI YA WABUNGE HUVUTA BANGI NA UNGA, ASEMA VIFAA MAALUM VITAFUNGWA ILI KUWABAINI
Kama unashangaa
kusikia kwamba aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga,
ametimuliwa kwa kuingia bungeni akiwa amelewa.
Bila shaka utachoka
zaidi ukisikia kuna wabunge kadhaa huingia kwenye ukumbi wa Bunge wakiwa
wametumia vilevi vikali zaidi vikiwamo bangi, viroba na dawa za kulevya.
Sunday, 22 May 2016
FAHAMU FAIDA ZA KULA TUNDA LA PAPAI KIAFAYA

Asili ya mpapai ni Amerika ya Kati,
ambapo kuanzia matunda, majani na utomvu wa mmea huu hutumiwa kama dawa maeneo
mbalimbali duniani. Vile vile, matunda na utomvu wake yamekuwa yakitumika
kutengeneza pombe na mvinyo katika baadhi ya nchi, huku wengine wakitumia
mpapai kama dawa kwa mifugo na binadamu.
MGODI WA DHAHABU WA GEITA NA TACAIDS WAZINDUA KAMPENI INAYOLENGA KUPIGA VITA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI
Saturday, 21 May 2016
MAREKANI YATOA SALUTI KWA WAPIGANAJI WA TANZANIA, YAMTUNUKU NISHANI YA ULIPUAJI WA MIZINGA MEJA JENERALI JAMES MWAKIBOLWA
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani linaloshughulikia
masuala ya kijeshi barani Afrika, Meja Jenerali Darrly Williams, amemtunuku
mkuu wa majeshi ya vikosi vya nchi kavu Tanzania Meja Jenerali James Mwakibolwa
nishani ya ulipuaji bora wa mizinga nchini.
MTOTO AMUUA MAMA YAKE NA KISHA KUMTUNDIKA DARINI
Mkazi wa Kitongoji cha
Kapembo, Kijiji cha King’wangoko wilayani Kaliua, Mkoa wa Tabora, ametiwa
mbaroni akituhumiwa kumuua, mama yake mzazi , Kiziko Lukambwe kwa
kumnyonga kisha kumtundika ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi.
MAONI YA ZITTO KABWE BAADA YA RAIS MAGUFULI KUMFUTA KAZI CHARLES KITWANGA
Habari kubwa iliyoteka
vyombo mbalimbali vya habari jana usiku ni habari ya Rais Magufuli Kumfuta kazi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga
UFAFANUZI WA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUHUSU KUTENGULIWA KWA KITWANGA
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais
Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw.
Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi
kulewa akiwa kazini.
TAREHE 20 MWEZI MAY RAISI MAGUFULI ALITENGUA UTEUZI WA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles
Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.
Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha
Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
20 Mei, 2016
NI MIAKA 20 SASA TANGU KUTOKEA KWA AJALI YA MELI YA MV BUKOBA.
Friday, 20 May 2016
JUMLA YA WADAIWA 21,721 WAJITOKEZA HESLB KUREJESHA MIKOPO
Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya
Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Robert Kibona akiongea
na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa agizo la siku 60
kwa wadaiwa wa Bodi hiyo na waajiri, ambapo takribani asilimia 72 ya wadaiwa
wote wameshawasilisha taarifa zao. Kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano
wa Bodi hiyo.
Mkurugenzi
Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya
Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Cosmas Mwaisobwa (kushoto) akieleza
kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)
kuhusu utaratibu wa urejeshaji wa mikopo kwa wadaiwa ambao mikopo yao
imeshaiva. Kulia ni Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya
Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Robert Kibona
JESHI LA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM LAFANIKIWA KUMKAMATA TAPELI WA MADINI
Kamanda wa Polisi
kanda maaalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro akionesha waandishi wa
habari mzani unaodaiwa kutumiwa na tapeli wa madini kupima madini bandia na
kuwatapeli wananchi wakati wa kutoa taarifa ya kukamatwa kwa tapeli huyo Jijini
Dar es salaam Mei 20 2016.
WIZARA YA NISHATI YATENGEWA TRIL.1.22/- KATIKA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2016/17
Wizara ya Nishati na
Madini imetengewa Sh trilioni 1.22 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 huku
fedha za miradi ya maendeleo zikiwa ni asilimia 94 ya fedha hizo.
Subscribe to:
Posts (Atom)