Tuesday 10 May 2016

WANANCHI WILAYANI BUKOMBE WASHAURIWA KUTUNZA MAZAO YA VYAKULA

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bukombe  mkoani Geita James  Ihunyo amewaomba  madiwani kuwaelimisha wananchi namna na jinsi wanavyotakiwa kuhifadhi  chakula ambacho kimepatikana  kwa wingi katika msimu  wa mavuno wa  mwaka  2015/2016.

Hayo ameyasema wakati wa kikao cha   baraza la   madiwani  wa kata zote  katika  halmashauri  hiyo kilichokuwa na lengo la kupokea  taarifa za kata na namna na jinsi ambavyo kata hizo zimeweza kufanya kazi kwa muda wa miezi  mitatu.

Ihunyo amesema  kuwa kutokana  na wimbi la wafanyabishara wanunuzi wa mazao kuvamia  wilaya   kumekuwepo na msongamano  wa  maroli yanayofika   vijijini huko  kununua nafaka na mazao aina ya mikunde  hali  ambayo imekuwa ikipelekea wananchi kujisahau na mwisho wa siku kuuza mazao yote na wao kubaki hawana chakula ndani.

Aidha  mbunge wa jimbo la Bukombe ,mh Dotto Biteko amewaomba  madiwani  kuendelea kumuunga mkono rais John Magufuli katika mikakati yake ya  kufanya mabadiliko  ya kweli kwa kuwa  hadi sasa nidhamu  kwa  watumishi  imeanza kuonekana.

No comments:

Post a Comment