Thursday 19 May 2016

WATU WATATU WAMECHINJWA KIKATILI NA WATU WASIOJULIKA NA KUPOTEZA MAISHA KATIKA MSIKITI WA RAMADHANI MKOLANI JIJINI MWANZA










Watu watatu wamefariki dunia papo hapo baada ya kuchinjwa na watu wasiojulikana katika mtaa wa Utemini Ibanda, Relini kata ya Mkolani jijini Mwanza.

Tukio hilo la kinyama limefanyika majira ya saa 2 usiku wa kuamkia leo wakati watu hao wakiwa msikitini wanasali katika msikiti wa Masjid Rahman, Kamanda wa polisi mkoani humo, Ahmed Msangi amethibisha kutokea kwa tukio.

Matukio ya watu kuuwawa kikatili yameendelea kushika kasi zaidi mkoani Mwanza licha ya jitihada mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la polisi huku wengine waikuwa kwa kukatwa na mapanga.

No comments:

Post a Comment