Thursday 5 May 2016

WADAU MKOANI GEITA WATAKIWA KUWASAIDIA WATOTO YATIMA...SIO KUSUBIRI SERIKALI PEKEE

 
Wadau  mbalimbali mkoani   Geita   wametakiwa kuwasaidia  watoto  yatima  na  wale  waishio katika mazingira  magumu  na sio kuiachia serikali  pekee.

Hayo  yamesemwa  na  diwani  wa  kata  ya Buhalahala  Musa Kabese wakati alipokuwa akikabidhi  sare  za shule kwa wanafunzi  waishio katika mazingira magumu katika  shule  za msingi Mwatulole,, Nguzo mbili,, na Buhalahala ikiwa ni moja ya ahadi zake alizoahidi kipindi cha kampeni.

Akitoa shukrani kwa niaba ya walimu,,  mwl mkuu wa shule ya msingi Mwatulole Catherini Mgusi  amesema kuwa msaada huo utawasaidia  watoto kujumuika na wenzao vizuri kwani hapo awali walikuwa wakivaa sare zilizochakaa na kuonyesha  baadhi ya sehemu za miili yao kitendo kilichowafanya watoto hao kujisikia aibu.

kwa upande  wake mwenyeki wa shule hizo Lucas  Kidengana amewaomba  wafadhili kuisaidia shule hiyo ili waweze   kutatua changamoto  mbalimbali zinazoikabili shule  hiyo  .


Aidha kwa upande wa wanafunzi wa shule hizo wametoa shukrani zao baada ya kupokea msaada huo ambapo wamemuomba diwani Kabese kusaidia kutatua na matatizo mengine yanayokabili shule hizo.

No comments:

Post a Comment