Tuesday 17 May 2016

UMBALI WA MAKAZI NA SHULE KWA BAADHI YA WANAFUNZI WA KIKE MKOANI GEITA BADO NI CHANGAMOTO,



Umbali wanaotumia wanafunzi wa kike kufata elimu ni sababu ambayo imeonekana kuendelea kudhorotesha elimu wanayoipata kwani wengi wao wamekuwa wakishawishiwa na mwisho wa siku kujikuta wakijiingiza katika mahusiano ya kimapenzi.
Wakizungumza na Storm habari baadhi  ya wanafunzi wa kike wa shule ya sekondari ya Kagu, wamesema kuwa umbali ambao wamekuwa wakitumia kutembea kutoka nyumbani  kwenda  shuleni ni sababu ambayo imekuwa ikipelekea kwa wanafunzi wengi kushindwa kutimiza ndoto zao.

Aidha wanafunzi hao wameiomba Serikali kutilia mkazo kwa shule za vijijini hususani za Sekondari kujenga hostel ambazo zitasaidia kuwanusuru na changamoto ambazo wamekuwa  wakikutana nazo mara  kwa  mara.


Mkuu wa shule hiyo Bw.Kilacha Nyamsogoro, amesema kuwa  hadi sasa jitihada ambazo walizifanya wazazi kuwapangishia watoto hao karibu na makazi ya shuleni hapo huku akielezea jitihada za kupatikana kwa mabweni.

No comments:

Post a Comment