Wednesday 25 May 2016

USAJILI WA WAFANYAKAZI WA UMWAGILIAJI DAWA ZA UKOKO WAINGIA DOSARI MKOANI GEITA


Wananchi  mkoani  Geita wamelalamikia kuwepo kwa tabia ya kuchukuliwa watu  wa  mikoa  ya  nje  katika zoezi la usajili wa wafanyakazi wa umwagiliaji dawa za viuatilifu vya mbua.

 Wakizungumza na Storm habari ambayo ilifika na kujionea  mwitikio  wa wananchi waliojitokeza kufanya usaili kwa ajili ya zoezi la umwagiliaji dawa za viutilifu,wamesema kuwa usajili umeonekana kuwa ni batili kutokana na kwamba,wasimamizi wa zoezi hilo wamekuja na watu kutoka nje na kwamba nii vyema zoezi hilo likaahilishwa kwani  wale wote ambao wamechaguliwa si wakazi wa eneo la mkoa wa Geita.

Kutokana na kuwepo kwa malalamiko hayo Storm habari ilifanikiwa kuzungumza na wenyeviti wa mitaa ambao ndio walikuwa wanafanya zoezi la kuwaandikisha wananchi hao,wamesema kuwa kutokana na kuwepo na ubatili katika zoezi hilo  ni   vyema likasitishwa  ili  usahili huo ufanyike kwenye  nganzi  ya mitaa.
  
Kutokana na kuwepo kwa malalamiko hayo Storm habari ilibidi imtafute ,afisa afya wa halamashauri ya mji,Mabela Mabela,lakini aligoma kuzungumza kwa madai kuwa anahitaji kupatiwa kibali na mkurugenzi.


Kutokana na majibu hayo Storm habari ilifika katika ofisi za mkurugenzi lakini haikubahatika kumkuta baada ya kuambiwa kuwa amekwenda kwenye kikao cha mkuu wa mkoa,na ilipo jaribu kuzungumza nae kwa njia ya simu alitoa kibali lakini afisa afya akaendelea kugoma na mwisho wa siku aliondoka.

No comments:

Post a Comment